Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa
Balozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani
Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KataviSaturday, January 30, 2016
MNADHIMU MKUU WA JWTZ,BALOZI WA TANZANIA KUWAIT,KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA WAAPISHWA RASMI NA RAIS WA JAMHURI WA TANZANIA DKT JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.
Friday, January 29, 2016
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO PROFESA MAKAME MBARAWA AKAGUA ATHARI ZA BARABARA MORO – DODOMA.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy
Ntenga akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri huyo
akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad
Chimagu (kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za barabara ya
Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
LHRC YAITAKA SERIKALI KUHESHIMU HAKI YA WATANZANIA KUPATA TAARIFA, YALAANI WABUNGE KUDHALILISHWA NA MBWA WA POLISI
Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi
habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo
kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.
Thursday, January 28, 2016
SERIKALI YA TANZANIA KUAHIDI KUJENGA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI.
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi
wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha
kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng Godwin
Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali
kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya ubovu wa
barabara nchini.
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO TAARIFA KWA UMMA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA UMMA
KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA - KOGA - TABORA
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda - Koga - Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo.
Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.
Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016
Tuesday, January 26, 2016
TRA YAOMBA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WANANCHI.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa
za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu
ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na
kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
WATUMISHI WA UMMA WATANGAZIWA KIAMA KWA WALE WATAKAOKIUKA TARATIBU NA SHERIA NA KUPOKEA RUSHWA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na wanahabari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.
Monday, January 25, 2016
TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 25 JANUARI 2016
Wizara yangu
inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa
kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu 14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa
pekee ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko
huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa mujibu wa Takwimu
za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa ambayo
imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo
idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10 vimeripotiwa. Idadi ya wagonjwa
walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki iliyoishia
tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621
na vifo 14 ambalo ni punguzo la
asilimia (16%). Mkoa wa Morogoro bado umeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi
ya wagonjwa ukilinganishwa na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89,
Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero 17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na
Ilemela 13), Simiyu (Bariadi DC 29
na Bariadi municipal 23), Manyara
(Simanjiro 48), Mara (Musoma Manispaa
11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita
(Geita DC 21 na Geita TC 6) na Mbeya (Kyela 26).
Mikoa mingine ambayo
bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Dodoma
(Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7),
Kilimanjaro (6) na Kagera (2).
RAIS ATENGUA WA BWANA DICKSON MAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA).
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
Sunday, January 24, 2016
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA WAMSHUKIA MHE MEMBE KWA MADAI KUWA AMEBEZA JUHUDU ZA RAIS WA AWAMU YA TANO.
Ally S. Hapi, Katibu Wa Idara,
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU
Elimu, Utafiti Na Uongozi,
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu waandishi wa
habari, nimewaita hapa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na kauli za hivi
karibuni za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Bernard Membe. Akifanya
mahojiano na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 22 na 23 Januari, 2016
, ndugu Membe amekaririwa akitoa kauli zenye maudhui ya kubeza juhudi za mh.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kufutwa kwa
uchaguzi wa Zanzibar. Kauli hizi zilijikita katika maeneo makubwa manne kama
ifuatavyo:-
Saturday, January 23, 2016
WATAALAMU DAWASCO WAKIENDELEA NA UKARABATI WA BOMBA LA MAJI MAENEO YA WAZO -TEGETA.
Kazi ya Kuunganisha Bomba la Maji kutoka mtambo wa uzalishaji wa Ruvu Chini ukiendelea katika eneo la Wazo Tegeta .
Matengenezo ya Bomba hili ndiyo yaliyopelekea kuzimwa kwa mtamb wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ambapo kwa muda wa saa 48 huduma ya maji itakosekana katika jiji la Dar Es Salaam na Bgamoyo.
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian
Luhemeja a-kizungumza juu ya
matengemezo hayo alipotembelea katika eneo hilo kujionea shughuli
zinavyoendelea.
Friday, January 22, 2016
SERIKALI IMNEJIKITA KUTOA ELIMU YA UZALISHAJI NA MATUMIZI ENDELEVU YA RASLIMALI.
Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George
Pangawe akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu wananchi
kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji nchini pale wanapotaka
kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka
Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni Mkuu wa Idara ya Mipango
Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara
Mkuu wa Kitengo cha Elimu
ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta akizungumza na
Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi
endelevu ya rasilimali ili waweze kunufaika na rasilimali hizi ambapo elimu
hiyo imeingizwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kulia ni Msaidizi Idara ya
Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George
Pangawe.
RAIS WA JAMHURII YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIWA AMEVALIA SARE ZA KIJESHI AKIWASALIMIA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Thursday, January 21, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMESEMA KUWA WANANCHI WANAANGALIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) MAANA NDIYO KITOVU CHA NCHI.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.
“Hapa ndiyo kitovu
cha nchi na Watanzania wote macho yao yako huku. Kwa nini? Kwa sababu huduma
zinasowagusa za barabara, maji, elimu, zinatokea huku kwa maana ya bajeti na
usimamizi,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo
(Alhamisi, Januari 21, 2016) wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa
taasisi na watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwenye mkutano uliofanyika
ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEWASILI MKOANI ARUSHA NA TAREHE 23 ATATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI WA KUNDI LA 57/15.
JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
KURUGENZI YA
MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 21 Januari, 2016 amewasili Mkoani Arusha ambapo keshokutwa tarehe 23
Januari, 2016 atatunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa kundi la 57/15
katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli mkoani hapa.
Rais Magufuli amewasili Mjini Arusha akitokea Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es salaam
na kupokelewa na mamia ya wananchi.
Akiwa uwanjani hapo Rais Magufuli amewashukuru wananchi kwa mapokezi
makubwa aliyoyapata na amewaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi
tu."Nawashukuru sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba
kuwahakikishia kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu"
Alisema Rais Magufuli.
Akiwa njiani kutoka uwanja wa ndege wa KIA, Rais Magufuli amesimamishwa
na wananchi wa njiapanda ya KIA, Kikatiti, Usa River, Tengeru na Mount Meru
Mjini Arusha ambapo huko kote pamoja na kusisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na
kilichobaki ni kuchapa kazi, amewahakikishia kuwa hatawaangusha.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee
kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni
yake ya kutumbua majipu.
"Nataka niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote
mpaka yaishe, na naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa
mafanikio" Alisisitiza Mheshimiwa Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema tayari serikali imeanza kutoa fedha kwa
ajili ya kugharamia elimu ya Msingi na Sekondari baada ya kufuta ada na akaonya
kuwa watumishi wa umma hususani wakuu wa shule watakaothubutu kufanya
ubadhilifu wa fedha hizo watashughulikiwa.
Amesema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania
kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na
kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania
kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao
na kanda zao na kuwataka watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na
kushirikiana kuiendeleza.
Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.
21 Januari, 2016
MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) IMEANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI KAMA UTARATIBU MPYA WA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA.
Mkurugenzi wa
Tafiti,Tathmini na Sera wa Mamalaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii Bw. Ansgar Mushi akitoa wito kwa wanachama wa Mifuko ya hifadhi za
jamii kote nchini kutohama mfuko wanaokuwa wanachangia mara wanapohama kutoka
Taasisi moja kwenda nyingine.
Afisa Tehama toka
Mamalaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Bw. Ernest
Masaka akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa mamalaka hiyo kupokea
malalamiko kutoka kwa wateja wa mifuko ya hifadhi za jamii kwa njia ya mtandao
wa simu kupitia namba 0762440706 ambapo mamlaka hiyo imepanua wigo wa
kushughulikia matatizo ya wanachama kwa wakati muafaka mara
yanapowasilishwa.kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi. Agnes Lubuva na
Kushoto ni Mkurugenzi wa Tafiti,Tathmini na Sera wa Mamalaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
Bw. Ansgar Mushi
Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) imeanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki kama utaratibu mpya wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
Akiongea na waandishi wa habari jijini dar es salaam afisa wa
Tehama mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii Bw.
Ernest Masaka amesema Utaratibu huo ni rahisi kutumia, Pia inaokoa muda na
nauli pamoja na kuboresha kuboresha Huduma kwa wanachama pale walipo kwa
kuongeza ufanisi ambapo amewataka wananchi na wanachama kwa ujumla kutumia
mfumo huo.
Aidha Bw.Masaka amesema mfumo huo umeweka utaratibu kwa mlalamikaji
pamoja na kutoa taarifa za malalamiko ya wanachama kwa vigezo vya aina ya
malalamiko kwa idadi na hatua ya utekelezaji kama ilivyofanyika.
Uanzishwaji wa mfumo huo ni hatua zinazochukiliwa na mamlaka
hiyo kwa lengo la kutetea maslahi ya wanachama Au Mwananchi yeyote kutoa
malalamiko au maoni kuhusu masuala ya sekta ya hifadhi ya jamii ikiwa ni
njia ya kuboresha sekta hiyo.
HUDUMA ZA WAGONJWA WA NJE KUBORESHWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.
Na Anaseli Stanley,
Hospital ya Taifa ya Muhimbili
imeboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa nje ili kusaidia wagonjwa kupata
Huduma kwa wakati pamoja na kupunguza msongamano katika eneo moja
ndani ya hospital hiyo.
Hayo
yameelezwa jijini Dar es salaam Na Mkuu wa idara ya Huduma ya wagonjwa wa nje
Dr. Raymond Mwenesano ambapo amesema kuwa wagonjwa watapata muda zaidi wa kutibiwa na kupata ushauri wa madaktali bingwa katika kliniki mbalimbali ambapo
awali kliniki zilikuwa hazitoi Huduma kwa kiwango kisichoridhisha kutokana na
kutokuwepo kwa muda wa kutosha.
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika
maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini ya jiji la Dar es salaam,
pamoja na baadhi ya maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana
na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 48 kuanzia siku ya Jumamosi 23/01/2016
hadi Jumapili 24/01/2016.
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) LAAGIZA MAPATO YAKUSANYWE KWA NJIA YA YA ELEKTRONIKI.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano Prof. Faustin
Kamuzora alifanya ziara ya kutembelea Shirika la Posta Tanzania ili kufahamu
utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Shirika.
Wednesday, January 20, 2016
MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA NEC LIMEFUNGULIWA NA MWENYEKITI WA TUME HIYO JAJI DAMIAN LUBUVA
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
ambaye ni mgeni rasmi wa mkutano huo, akiongea na Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini
Dar es Salaam kuhusu masuala ya maadili na na ufanisi kazini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana
Ramadhani Kailima akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo
pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhusu
masuala ya maadili na na ufanisi kazini kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi.
BALOZI SEIF ALI IDD AKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU NA KUMDHIBITISHIA KUWA KUNA AMANI ZANZIBAR NA WANASUBIRI TAREHE YA UCHAGUZI ITANGAZWE RASMI.
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri
kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.
Sunday, January 17, 2016
GAZETI LA MAWIO LAFUNGUWA MOJA KWA MOJA NA SERIKALI.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu anayenyoosha mkono)
akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa
kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana
na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa
pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw.
Raphael Hokororo na anayemfuatia ni Mwanasheria wa Wizara Bw. Patrick Kipangula
Friday, January 15, 2016
UJENZI WA SHULE NI JUKUMU LA WADAU MBALIMBALI KUSHIRIKI KATIKA KUKAMILISHA SUALA HILO.
Na Anaseli
Stanley,
Mkuu wa
wilaya ya kinondoni bw. Paul Makonda amewataka wadau na makampuni mbalimbali
kuendelea kusaidia azimio la ujenzi wa shule saba katika wilaya hiyo kwa lengo
la kusaidia watoto zaidi ya elfu 3 ambao wana uhitaji wa elimu ya sekondari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dare s salaam wakati akipokea misaada hiyo Bw.
Makonda amesema kuwa anawashukuru wadau hao na kuwataka wengine kujitokeza
kusaidia kukamilisha kwa zoezi hilo la ujenzi
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROF. SOSPETER MUHONGO AMEIAIGIZA KAMPUNI YA UENDELEZAJI JOTOARDHI TANZANIA (TGDC LTD) KUWA IFIKAPO JUNE 2016, IWE IMEANZA KUCHORONGA MASHIMO 3 KATIKA ENEO LA ZIWA NGOZI.
WAZIRI wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameiaigiza Kampuni ya
Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC Ltd) kuwa ifikapo June 2016, iwe
imeanza kuchoronga mashimo 3 katika eneo la Ziwa Ngozi ikiwa ni hatua ya mwisho
inayohitajika kabla ya kuanza kujenga mitambo ya kuzalisha jotoardhi.
WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WANATARAJIA KUFANYA UZINDUZI WA STIKA MAALUM JANUARI 26,
Na Nyakongo Manyama-MAELEZO
TAASISI ya watu wenye ulemavu wa
ngozi mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa ‘stika’ maalum
yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye albinism utakaofanyika januari
26 mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Michael Lugendo amesema kuwa uzinduzi huo
utafanyika katika kituo cha polisi kati jijini Dar es Salaam kuanzia saa tano
asubuhi.
HUDUMA ZA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA HAPA NCHINI ZIMEKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEPO NA WATOA HUDUMA WASIOZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO MBALIMBALI.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
MAELEZO YA WAZIRI KUHUSU
TIBA ASILI NA TIBA MBADALA
Ndugu Wananchi, Katika nchi yoyote
ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na
wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na
mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau.
Huduma za tiba asili
na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina
thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa.
Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo
mbalimbali.
SERIKALI IMEWATAKA WAWEKEZAJI WA TANZANIA KUUNGANA NA WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA KUINUA WIGO NA KUJENGA UZOEFU
Na, Anaseli Stanley.
Serikali imewataka wawekezaji wa Tanzania
waungane na wawekezaji wa mataifa mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu na
kufanya kazi nyingi za serikali hapa nchini ili makampuni ya Tanzania yawe na
uwezo wa kutenda kazi kubwa na kuongeza kipato kwa taifa.
Hayo yameelezwa mbele ya waandishi wa
habari jijin dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wakandarasi wa japani na
watanzania wazziri mkuu MH.Kasim Majaliwa amesema kuungana huku kutsaidia
kubadilishana mawazo na kujadili namna mbalimbali za uendeshaji wa makampuni ya
ndanina kuongeza ushindani na mataifa mengine.
Wednesday, January 13, 2016
MAHABUSU YA WATOTO JIJINI DAR ES SALAAM YAPEWA VITU MBALIMBALI NA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam Bw.
Ramadhan Yahaya (kulia) akipakua msaada wa vyakula na vitu mbalimbali
vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu
ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw.
WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WANAOSOMA KATIKA VYUO MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2015 NA 2016 WAKUMBUKWA NA BODI YA MIKOPO.
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetoa jumla
ya sh bilioni 459 fedha za kitanzania kwa wanafunzi wa elimu ya juu 122,486
wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi katika mwaka wa masomo
2015/2016.
Hayo yameelezwa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano
Omega Ngole amesema kuwa hiyo ni idadi kubwa ya wanafunzi walionufaika na mkopo
huo tangu kuanzishwa kwa bodi mwezi julai 2005.
‘’Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali
kupitia bodi ilitoa jumla ya tsh bilioni 341 ziliwanufaisha wanafunzi 99,069
alisema’’.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFIKA NA KUFARIJI FAMILIA YA BABA WA TAIFA KUFUATIA MSIBA WA MBUNGE WA ZAMANI CHADEMA LETICIA NYERERE NA PIA KUMTEMBELEA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TATU MHE.SUMAYE KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akitia saini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa zamani,Leticia mageni
Nyerere wakati alipokwenda kumhani mjane wa Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere
Msasani jijini Dar es salaam Januari 12, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, January 11, 2016
KWA MUJIBU WA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MAALIM SEIF HAMAD AMESEMA KURUDIWA UCHAGUZI ZANZIBAR ITASABABISHA MACHAFUKO VISIWANI HUMO.
Aliyekuwa mgombea urais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa kutokana na mgogoro
wa kisiasa unaoendelea visiwani humo usipopatiwa ufumbuzi mara moja na
kulazimisha kuwa uchaguzi huo urudiwe nidhahiri kuwa hatua hiyo inalazimisha
kuwepo kwa hali ya machafuko visiwani humo.
Saturday, January 09, 2016
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Nchi yetu ina kingo za mito na
mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku
wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao. Kutokana na uhaba wa
makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde
la Mto Msimbazi.
ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA KATOLIKI LA DAR ES SALAAM, MWADHAMA POLYCARP KARDINALI PENGO AMEPONGEZA WELEDI WA HUDUMA YA TASISI YA MOYO ILIYOPO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kupongeza jopo la
Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
Friday, January 08, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU VIKAO VYA TATHMINI NA UCHAMBUZI VYA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Katika
utaratibu wake wa kujipanga na kuendelea kutekeleza mikakati ya malengo ya muda
mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kufikia lengo kuu la kushinda uchaguzi,
kushika dola na kuongoza serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa na utamaduni wa kuwa na vikao vya
kujitathmini na kufanya uchambuzi kila baada ya uchaguzi mkuu na kuweka mpango
kazi unaopaswa kutekelezwa na chama kwa miaka mitano inayofuata.
PICHA RASMI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI INAPATIKANA IDARA HABARI MAELEZO KWA SHILINGI 15,000.
Thursday, January 07, 2016
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 07 JANUARI, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)