Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na
watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro.Waziri huyo amefika
katika kituo hicho ili kujionea hali ya
kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na
jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu
Showing posts with label WAZIRI WA AFYA. Show all posts
Showing posts with label WAZIRI WA AFYA. Show all posts
Monday, July 10, 2017
Thursday, March 16, 2017
UMMY MWALIMU ATOA MIEZI MITATU KUANZISHWA DUKA LA DAWA
Wednesday, March 08, 2017
MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA MKOANI SINGIDA

Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua kituo na kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UN women Tanzania Maria Karadenizli.
Friday, January 20, 2017
Thursday, December 15, 2016
Friday, October 07, 2016
WAZIRI UMMY ATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.
Thursday, October 06, 2016
Monday, April 25, 2016
WAZIRI UMMY MWALIMU AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUPIMA MALARIA KWA KUTUMIA MRDT:
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.
Friday, April 08, 2016
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD KANDA YA MBEYA.
Na Rabi Hume.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa.
“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
Friday, January 15, 2016
HUDUMA ZA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA HAPA NCHINI ZIMEKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEPO NA WATOA HUDUMA WASIOZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO MBALIMBALI.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
MAELEZO YA WAZIRI KUHUSU
TIBA ASILI NA TIBA MBADALA
Ndugu Wananchi, Katika nchi yoyote
ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na
wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na
mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau.
Huduma za tiba asili
na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina
thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa.
Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo
mbalimbali.
Subscribe to:
Posts (Atom)


