Friday, January 15, 2016

SERIKALI IMEWATAKA WAWEKEZAJI WA TANZANIA KUUNGANA NA WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA KUINUA WIGO NA KUJENGA UZOEFU

Na, Anaseli Stanley.
Serikali imewataka wawekezaji wa Tanzania waungane na wawekezaji wa mataifa mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu na kufanya kazi nyingi za serikali hapa nchini ili makampuni ya Tanzania yawe na uwezo wa kutenda kazi kubwa na kuongeza kipato kwa taifa. 

Hayo yameelezwa mbele ya waandishi wa habari jijin dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wakandarasi wa japani na watanzania wazziri mkuu MH.Kasim Majaliwa amesema kuungana huku kutsaidia kubadilishana mawazo na kujadili namna mbalimbali za uendeshaji wa makampuni ya ndanina kuongeza ushindani na mataifa mengine.

Aidha mh. majaliwa ameongeza kusema kuwa serikali itatoa nafasinyi nyingi za kufanya kazi kwa wakandarasi wa ndani japo uwezo wa wakandarasi hao bado unaendelea kuimarika lakini wataweza kuongeza ushindani

nae naibu waziri wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano injinia Edwini Ngonyani akawataka wakandarasi hao kuwa na umoja na ukuribu na wajapani hao ambao huwa wanapewa miradi mingi kutoktana na uzoefu walionao ili wanapopewa miradi washirikiane nao.

katika miradi hiyo ya ujenzi hapa nchiniwawekezaji na wakandarsi wa nje na ndani wamekutana na kujadili kwa pamoja ili kujaribu kutafuta mbinu mbalimbali za kutatua changamoto za miundimbinu ambapo pia ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya makutano ya barabara zikiwekewa mipango madhubuti ya kuweza kupunguza foleni katikta jiji la Dar es salaam hasa maeneo ya tazara na ubungo.


No comments:

Post a Comment