Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa
za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu
ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na
kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba
wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu
ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema
Kayombo.
Mkurugenzi
Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689122515 au
kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516 na
kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa
kazi.
Aidha
Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna
mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na
maadili.
TRA
kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani imepokea malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia
uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.
No comments:
Post a Comment