Aliyekuwa mgombea urais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa kutokana na mgogoro
wa kisiasa unaoendelea visiwani humo usipopatiwa ufumbuzi mara moja na
kulazimisha kuwa uchaguzi huo urudiwe nidhahiri kuwa hatua hiyo inalazimisha
kuwepo kwa hali ya machafuko visiwani humo.
Kauli ya Maalim Seif imekuja muda mfupi wakati akiongea na
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuwaeleza ni namna gani hali ya
kisiasa visiwani humo ilivyo na mazungumzo waliokuwa wakizungumza walipofikia
hadi hivi sasa.
Amesema hali ya kisiasa bado tete kwakuwa vikao 8 walivyo kaa hadi
sasa vimekuwa vya matumaini bila maridhiano yakina na kufikia muafaka ambao
umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na wananchi pamoja watu mbali mbali viwani humo
hali ambayo imekuwa ikizusha maswali yakuwa kwanini mazungumzo hayo
hayakamiliki kwa wakati.
Kutokana na hatua hiyo sasa amemtaka rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kuongoza mazungumzo ya kutatua mgogoro wa
kisiasa unaoendelea visiwani humo kwa kufuata misingi ya kikatiba na sheria baada
ya mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati yake na Dr Ali Mohamed Shein kwa
kuwashirikisha marais wastaafu wa Zanzibar kutoonesha kuzaa matunda.
Hata hivyo katika mazungumzo ya Maalim Seif juu ya majadiliano
hayo ya kutafuta muafaka amemshutumu Dr Ali Shein kwa kusema kuwa hakua na nia
njema na mazungumzo hayo na hivyo amepoteza sifa ya kuongoza mazungumzo
hayo,huku akisema anazo taarifa kuwa tume ya uchaguzi imepanga kukutana January
ili kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi huku wananchi wa Zanzibar wakiwa wako
taaban na wamekumbwa na fadhaa baada ya kuona maamuzi yao yanakanyagwa bila
muafaka.
Pia Maalim ameendelea kwenda mbali zaidi akisema kuwa kamwe tume
haina mamlaka ya kutengua matokeo bali ina mamlaka ya kurudia kuhesabu kura
hivyo jambo alilolifanya mwenyekiti wa tume Zanzibar Jecha Salim Jecha alienda
kinyume cha katiba kwa kufanya maamuzi bila kushirikiana na tume.
Katiba inasema "kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na
wajumbe walio wengi". Anasema katiba imetumia neno 'Lazima' na mwenyekiti
kwenda kinyume inafaa kuchukuliwa hatua,alisema Seif.
Ingawa mwenyekiti aliitisha kikao kuhalalisha maamuzi yake bado
tume haikuwa na mamlaka ya kuhalalisha maamuzi ya kufuta uchaguzi uliokamilika
na Tamko la mwenyekiti lilisema anafuta uchaguzi na matokeo yake yote hata
hivyo tangazo rasmi lilisema anafuta matokeo ya uchaguzi.
Vifungu vya katiba vilivyonukuliwa, vimenukuliwa kwa ubabaishaji
kuhalalisha uwezo wa tume kufututa matokeo kifungu cha 34 kimeweka utaratibu wa
kufunga kituo ikitokea dosari,sheria imetoa fursa ya wazi kwa mwenye malalamiko
na kwa mujibu wa sheria hakuna malalamiko yaliyowasilishwa mbele ya tume.
Tangu uchaguzi wa vyama vingi zianze zimekuwa zimekumbwa na kasoro
ukiwemo wa mwaka 2000 uliolazimu vituo 16 kurejea uchaguzi Zanzibar, hivi kweli
uchaguzi wa 2015 ulizidi kasoro za mwaka 2000.
Maalim amesema Tume haipaswi kupewa maagizo na chama chochote cha
siasa au chombo chochote, ni dhahiri maamuzi ya mwenyekiti yalikuwa ya maagizo
kama alivyowaeleza wenzake.
Athari za kufutwa kwa uchaguzi kumepelekea athari kadha za
kikatiba, mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisheria.
Imepelekea Zanzibar kuwa na mgogoro kwa Rais aliyeko madarakani,
washauri wametumia tafsiri isiyo sahihi ya kikatiba hadi Rais mpya
atakapoapishwa.
Mpaka wa kifungu kinachorusu mpaka Rais ajae atakapoapishwa ni
kuwa muda wa Rais ni miaka mitano pekee na katiba haijaruhusu muda wa miaka
mitano uongezwe kiholela ila kwa masharti mazito ikiwemo vita na Rais akaona ni
muhimu kusitisha uchaguzi basi ataitisha baraza la wawakilishi na linaweza
kumuongezea muda usiozidi miezi sita.
Tafsiri isiyokuwa sahihi ina athari zifuatazo
Haujawekwa muda maalum na katiba imeweka muda maalum kwa chaguzi
zinazofutwa kisheria, kwa maana hiyo hakuna ukomo mpaka uchaguzi utapoitishwa
tena.
Tafsiri hio haimpi fursa ya Rais kumuwajibisha mtu alienda kinyume
cha katiba kwa sababu imemnufaisha Rais. Tafsiri sahihi ni lazima Rais ashike
madaraka ya Urais na aachie nafasi hio baada ya miaka mitano isipokuwa kwa
dharura zilizopo kisheria.
Mgogoro wa kutokuwa na Rais halali tangu tarehe 3 November 2015 na
ameendelea kufanya maamuzi makubwa ikiwemo ya uteuzi.
Hata hivyo inasikitisha kuona mimi nikikubali kuwa kimya kipindi
chote, inasikitisha kuona viongozi wa upande mwingine wakiongea na
kuwachanganya watu.
Magufuli pamoja na juhudi zote hakuacha kufitinishwa kwa Balozi
Seif Ali Iddi kusema eti Magufuli kasema turudi Zanzibar kukamilisha taratibu
za kurudia uchaguzi ilhali mimi hakuniambia.
Hadi jana ukiangalia tovuti ya uchaguzi Zanzibar hadi jana inasema
uchaguzi ulifanyika kwa amani nchi nzima.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa Zanzibar imepita siasa za dhoruba
na machafuko kwa miaka 50 ndio maana yeye kwa mwaka 2009 sambamba na na Rais
mstaafu Karume walifikia maridhiano.
Wakati wa maswali kwa waandishi wa habari moja ya Swali
aliloulizwa na kutakiwa kulitolea ufafanuzi ni juu ya kuwa zipo taarifa kuwa
yeye sio Mzanzibari ambapo alisema kuwa “chaguzi tano nagombea urais na hakuna
mtu hata mmoja anaweka pingamizi, hata kumjibu ni kinyaa. Eti Zanzibar vyama vya
upinzani viruhusiwe kugombea nafasi zote kasoro Urais, wanaogopa nini? Wote ni
watanzania na wanaogombea kupitia vyama hivyo ni watanzania.
No comments:
Post a Comment