Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi
habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo
kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na
haki za binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza
kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa
kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima wananchi taarifa
muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.
Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake
lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine
hususani serikali.
Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge
kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,
Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna
Henga yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia
gharama hizo za matangazo ya bunge.
No comments:
Post a Comment