Friday, January 15, 2016

UJENZI WA SHULE NI JUKUMU LA WADAU MBALIMBALI KUSHIRIKI KATIKA KUKAMILISHA SUALA HILO.

Na Anaseli Stanley,
Mkuu wa wilaya ya kinondoni bw. Paul Makonda amewataka wadau na makampuni mbalimbali kuendelea kusaidia azimio la ujenzi wa shule saba katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia watoto zaidi ya elfu 3 ambao wana uhitaji wa elimu ya sekondari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare s salaam wakati akipokea misaada hiyo Bw. Makonda amesema kuwa anawashukuru wadau hao na kuwataka wengine kujitokeza kusaidia kukamilisha kwa zoezi hilo la ujenzi

Nao wadau hao wakasema wameguswa  na kuvutiwa na juhudi za kuendeleza elimu hivyo hawana budi kutoa kidogo walicho nacho ambapo pia wakawataka wazazi kuwapeleka watoto wao shule kutokana kufutwa kwa ada mashuleni na wao kama wadua wamaendeleo ya elimu wameamua kushiriki kuongeza shule kukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Mkuu wa wilaya huyo leo amepokea zaidi ya mifuko ya saruji 1000 na mabati 100 kama kianzio cha ujenzi huo kwa makampuni tofauti  ambapo pia akawataka wadau wangine kujitokeza kwa lengo la kusaidia kutimiza sera ya elimu bure ambapo haiwezi kuwa na tija kama kutakuwa hakuna shule za kutosha kwa wanafunzi hao kupata elimu hiyo.

No comments:

Post a Comment