Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Mkewe Mary (wapili kulia) wakiifariji familia ya Mjane wa Baba waTaifa,
Mama Maria Nyerere (kulia) wakati walipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa
Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa mbunge wa zamani, Leticia Nyerere,
Januari 12, 2016. Kushoto ni mtoto wa baba wa Taifa, Rose Nyerere na wapili
kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.
WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere.
Akizungumza na mama Maria alipomtembelea
nyumbani kwake Jumanne, Januari 12,2016), Msasani jijini Dar es salaam, Waziri
Mkuu ametoa pole kwa Mama Maria Nyerere pamoja na familia na
kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu baada ya
kuondokewa na mpendwa wao.
kuondokewa na mpendwa wao.
“Kipindi hiki ni kigumu, hatuna
budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia tutajumuika nanyi katika kipindi
hichi chote, tuendelee kuwa watulivu na kumwomba Mungu” alisema Waziri Mkuu
Majaliwa.
Ndugu wa marehemu, John Shibuda
(aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza kutokea kwa msiba huo. Ambapo
amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia Nyerere alipelekwa nchini Marekani kwa
matibabu na alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo
Lanham, Maryland juzi saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Aidha, Shibuda amemshukuru
Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole familia na Serikali kwa
namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa familia.
Naye, Rose Nyerere
amesema familia inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa taarifa ya baada ya
kuandaa utaratibu wa siku ambayo mwili utaletwa nchini, kuagwa na hatimaye
kuzikwa Butiama.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu mstaafu Frederick
Sumaye ambaye amelazwa siku kadhaa zilizopita katika Taasisi ya Jakaya Kikwete
iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa, amesema amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo mstaafu akiendelea vizuri na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kumpatia matibabu na kumhudumia vizuri. Pamoja na kumpa pole, Waziri Mkuu amemwombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Naye, Waziri Mkuu mstaafu
Fredrick Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kumtembelea hospitalini
hapo, pia ameipongeza Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya ili kusaidia
wananchi na hatimaye kuiletea nchi maendeleo.
“Naipongeza Serikali kwa namna
ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika masuala mbalimbali yenye
lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri Mkuu Majaliwa, pia
amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh ambaye amelazwa na
anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Picha na ofisi ya waziri mkuu,
No comments:
Post a Comment