Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetoa jumla
ya sh bilioni 459 fedha za kitanzania kwa wanafunzi wa elimu ya juu 122,486
wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi katika mwaka wa masomo
2015/2016.
Hayo yameelezwa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano
Omega Ngole amesema kuwa hiyo ni idadi kubwa ya wanafunzi walionufaika na mkopo
huo tangu kuanzishwa kwa bodi mwezi julai 2005.
‘’Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali
kupitia bodi ilitoa jumla ya tsh bilioni 341 ziliwanufaisha wanafunzi 99,069
alisema’’.
Kati ya fedha zilizotolewa jumla ya tsh bilioni 199.7
zilikwenda kwa wanafunzi wa masomo ya mwaka wa kwanza 53,537 na tsh 259.1
bilioni zililipwa kwa wanafunzi 68,916 wanaoendelea na masomo wa mwaka wa pili
na kuendelea katika vyuo vya umma na binafsi.
‘’Bwana omega ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya bdi
ya mikopo iliyotolewa kundi kubwa la
wanafunzi wanaopata mikopo ni wale wanaosoma program za kipaumbele ambazo ni
udaktari wa binadamu,udaktari wa meno,udaktari wa wanyama,ufamasia na uuguzi na
ualimu wa masomo ya sayansi na hesabu pamoja na yatima na walemavu.
Hata hivyo bodi ya mikopo inatoa wito kwa waajiri katika
taasisi za uma na binafsi nchni kuhakikisha wanazingatia sheria liyoanzishwa na
bodi hiyo inayowataka kutambua waajiriwa ambao ni wanufaika wa mikopo
inayotolewa na bodi ili kukata sehemu ya mishahara na kuiwasilisha kwa bodi
kama marejesho.
Ikumbukwe kuwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria no.9 ya mwaka
2004 na kuanza kazi mwezi juai 2005 ikiwa na majukumu ya kutoa mikopo kwa
wanafunzi pamoja na kusimama urejeshi wa mikopo kutoka kwa wanufaika wa mikopo
hiyo.
No comments:
Post a Comment