Showing posts with label Jiji la Dar es salaam. Show all posts
Showing posts with label Jiji la Dar es salaam. Show all posts

Saturday, May 21, 2016

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam , Willson Kabwe Afariki Dunia

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe ambaye April 19 mwaka huu alisimamishwa kazi na Rais Magufuli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na  Meya wa Jiji la Dar  es Salaam,Isaya Mwita

Kabwe amefikwa na mauti  akiwa nchini India kwa matibabu. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu. Amina

Monday, May 16, 2016

UKARABATI WA KIVUKO CHA MV MAGOGONI WAANZA RASMI.

tem1

Ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Magogoni umeanza rasmi mara baada ya kusitisha huduma zake hivi karibuni.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la bandari kujionea kazi ya ukarabati kwa kivuko hicho, Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole-kujan amesema kazi ya ukarabati wa kivuko hicho umeanza kwa hatua za awali za kukifanyia usafi ili kuona maeneo yaliyoharibika na kuyafanyia ukarabati.

Sunday, February 28, 2016

MWALIMU WA KIKE WA SHULE YA MSINGI MSIGANI JIJINI DAR ES SALAAM AUAWA KINYAMA KWA KUPIGWA RISASI.

Na Masau Bwire,
Mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 25 wa Shule ya msingi Msigani, Kimala Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumamosi saa 2 usiku!

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es salaam, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Christopher Sprian Fuime amesema mwalimu huyo aliuawa kwa kupigwa Risasi hiyo wakati akijiandaa kufunga kibanda chake cha biashara kilichopo pembeni mwa uwanja wa Shule anayofundisha.

Kamanda Fuime amesema, wauaji hao ambao walifika katika kibanda cha mwalimu huyo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki, walivunja kioo cha kibanda hicho, mmoja mwenye bastola akaingia ndani na kumpiga Risasi iliyomsababishia kifo papo hapo, kisha wao kuondoka bila kuchukua kitu  chochote!

Amesema juu ya meza katika kibanda cha biashara cha mwalimu huyo kulikutwa shilingi laki tatu, vocha za simu na simu kadhaa za mkononi ambazo hazikuguswa na watu hao, hali ambayo inalifanya Jeshi la Polisi lishindwe kubaini kwa haraka mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika sababu za mauaji hayo.

Kamanda Fuime amesema, Serikali kupitia Jeshi la Polisi itahakikisha hakuna jambazi anayepata ushindi na kufanya raia waishi kwa hofu katika nchi yao na kuongeza kwamba, kutoa uhai wa mtu kwa ajili ya Mali, chuki na uhasama ni vitendo ambavyo havitavumiliwa na Jeshi la Polisi, litapambana na watu wenye tabia hizo, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola.

Aidha Kamanda Fuime ametoa mwito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwezesha kupatikana na kukamatwa kwa watu hao na wahalifu wengine.

Saturday, January 09, 2016

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM




Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.