Showing posts with label Elimu. Show all posts
Showing posts with label Elimu. Show all posts

Monday, July 11, 2016

INDIA YAIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 500 ZA KIMAREKANI KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

India imeipatia Tanzania dola za Kimarekani milioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina nchi hizi mbili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake, Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi.
“Tunaishukuru India ambayo imeonyesha utayari wa kushirikiana nasi kiuchumi katika kilimo, TEHAMA, maji, Elimu, Afya na Ulinzi,” amesema Rais Magufuli.Rais Magufuli pia amesema ushirikiano wetu na India utatoa fursa kwa Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda kwani katika ziara hii Waziri Mkuu ameambatana na wafanyabiashara takriban 50 ambao wanaangalia fursa za kibiashara hapa nchini.

Sunday, January 24, 2016

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA WAMSHUKIA MHE MEMBE KWA MADAI KUWA AMEBEZA JUHUDU ZA RAIS WA AWAMU YA TANO.

 Ally S. Hapi, Katibu Wa Idara,
Elimu, Utafiti Na Uongozi,

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na kauli za hivi karibuni za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Bernard Membe. Akifanya mahojiano na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 22 na 23 Januari, 2016 , ndugu Membe amekaririwa akitoa kauli zenye maudhui ya kubeza juhudi za mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Kauli hizi zilijikita katika maeneo makubwa manne kama ifuatavyo:-