Thursday, January 21, 2016

MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) IMEANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI KAMA UTARATIBU MPYA WA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA.


Mkurugenzi wa Tafiti,Tathmini na Sera wa Mamalaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Bw. Ansgar Mushi akitoa wito kwa wanachama wa Mifuko ya hifadhi za jamii kote nchini kutohama mfuko wanaokuwa wanachangia mara wanapohama kutoka Taasisi moja kwenda nyingine.

Afisa Tehama toka Mamalaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Bw. Ernest Masaka akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa mamalaka hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa wateja wa mifuko ya hifadhi za jamii kwa njia ya mtandao wa simu kupitia namba 0762440706 ambapo mamlaka hiyo imepanua wigo wa kushughulikia matatizo ya wanachama kwa wakati muafaka mara yanapowasilishwa.kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi. Agnes Lubuva na Kushoto ni Mkurugenzi wa Tafiti,Tathmini na Sera wa Mamalaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Bw. Ansgar Mushi

Na Anaseli Stanley,
Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) imeanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki kama utaratibu mpya wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wake  na wananchi kwa ujumla.
Akiongea na waandishi wa habari jijini dar es salaam afisa wa Tehama mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya  hifadhi ya jamii Bw. Ernest Masaka amesema Utaratibu huo ni rahisi kutumia, Pia inaokoa muda na nauli pamoja na kuboresha kuboresha Huduma kwa wanachama pale walipo kwa kuongeza ufanisi ambapo amewataka wananchi na wanachama kwa ujumla kutumia mfumo huo.
Aidha Bw.Masaka amesema mfumo huo umeweka utaratibu kwa mlalamikaji pamoja na kutoa taarifa za malalamiko ya wanachama kwa vigezo vya aina ya malalamiko kwa idadi na hatua ya utekelezaji kama ilivyofanyika.
Uanzishwaji wa mfumo huo ni hatua zinazochukiliwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kutetea maslahi ya wanachama Au Mwananchi yeyote kutoa malalamiko au maoni  kuhusu masuala ya sekta ya hifadhi ya jamii ikiwa ni njia ya kuboresha sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment