Showing posts with label Elimu ya juu. Show all posts
Showing posts with label Elimu ya juu. Show all posts

Wednesday, January 13, 2016

WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WANAOSOMA KATIKA VYUO MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2015 NA 2016 WAKUMBUKWA NA BODI YA MIKOPO.

Na Jesca Mathew na Anaseli Stanley.
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetoa jumla ya sh  bilioni 459 fedha za kitanzania  kwa wanafunzi wa elimu ya juu 122,486 wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi katika mwaka wa masomo 2015/2016.
Hayo yameelezwa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano Omega Ngole amesema kuwa hiyo ni idadi kubwa ya wanafunzi walionufaika na mkopo huo tangu kuanzishwa kwa bodi mwezi julai 2005.
‘’Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali kupitia bodi ilitoa jumla ya tsh bilioni 341 ziliwanufaisha wanafunzi 99,069 alisema’’.