Showing posts with label rais Jakaya Kikwete. Show all posts
Showing posts with label rais Jakaya Kikwete. Show all posts

Friday, June 17, 2016

POLISI WAMUWINDA ASKOFU GWAJIMA KWA MASAA 7 BILA MAFANIKIO........NI BAADA YA KUSAMBAA KWA SAUTI INAYOSADIKIKA NI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII AKIMSEMA VIBAYA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE:

Polisi walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio. 

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.

Friday, June 03, 2016

UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKTABA YA KISASA, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.