Showing posts with label waziri mkuu Kasimi Majaliwa. Show all posts
Showing posts with label waziri mkuu Kasimi Majaliwa. Show all posts

Thursday, March 17, 2016

ZIARA YAWAZIRI MKUU, CHATO NA KATORO - GEITA.

 Waizri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kukamu mafuta ya alizeti  wanaushirika wa Chato akiwa

 katika ziara ya mkoa wa Geita Machi 17, 2016. Kushoto ni

 Mwenyekiti wa  Ushirika huo Elias Kaswahili. 

 Wasani wa Katoro Geita wakicheza ngoma ya Kisukuma

 mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia

 mkutano wa hadhara kijijini hapo  Machi 17, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro , Geita Machi 17, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, March 10, 2016

WAZIRI MKUU:TANZANIA YAINUKA KIUCHUMI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
 "Kumekuwa na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa mfumuko wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa limekua kwa wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 5.3 mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka 2013," alisema.

Friday, February 12, 2016

WATENDAJI WAKUU WA WAKALA WA VIPIMO NCHINI WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI WA UPOTEVU WA MAFUTA BANDARINI.

SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.

Thursday, January 21, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMESEMA KUWA WANANCHI WANAANGALIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) MAANA NDIYO KITOVU CHA NCHI.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.

“Hapa ndiyo kitovu cha nchi na Watanzania wote macho yao yako huku. Kwa nini? Kwa sababu huduma zinasowagusa za barabara, maji, elimu, zinatokea huku kwa maana ya bajeti na usimamizi,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 21, 2016) wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa taasisi na watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwenye mkutano uliofanyika ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma.