Thursday, January 21, 2016

HUDUMA ZA WAGONJWA WA NJE KUBORESHWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

Na Anaseli Stanley,
Hospital ya Taifa ya Muhimbili imeboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa nje ili kusaidia wagonjwa kupata Huduma kwa wakati pamoja na kupunguza msongamano  katika  eneo moja ndani ya hospital hiyo.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam Na Mkuu wa idara ya Huduma ya wagonjwa wa nje Dr. Raymond Mwenesano ambapo amesema kuwa wagonjwa watapata muda zaidi wa kutibiwa na kupata ushauri wa madaktali bingwa katika kliniki mbalimbali ambapo awali kliniki zilikuwa hazitoi Huduma kwa kiwango kisichoridhisha kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha.

Aidha Dr. Mwenesano amesema utaratibu huo utawahusu wagonjwa wanaokuja kutibiwa na kuondoka hususani waolipia fedha taslim,wagonjwa wote ambao ni wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya, bima mbalimbali za afya pamoja na watumishi ambao makampuni yao yanamikataba na hospitali kutibu wafanyakazi wao.

Kliniki hizo zinazofanyika katika hospital ya muhimbili sasa zinatolewa kila Siku kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 12. jioni Na siku ya jumamosi mpaka saa 8 mchana ambapo wananchi wametakiwa wafike hospitalini hapo ili kupata Huduma.


No comments:

Post a Comment