Showing posts with label JINSIA. Show all posts
Showing posts with label JINSIA. Show all posts

Monday, July 10, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA KATORO NA KUJIONEA HALI YA KITUO HICHO

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro.Waziri huyo amefika katika  kituo hicho ili kujionea hali ya kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu

Wednesday, April 19, 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni leo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2017. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, March 21, 2017

Kingwangala Ataja Sababu za Kutowataja Mashoga Hadharani

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga).

Thursday, March 16, 2017

UMMY MWALIMU ATOA MIEZI MITATU KUANZISHWA DUKA LA DAWA

Image result for picha za ummy mwalimuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza kuanzishwa duka la dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Wednesday, March 08, 2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA MKOANI SINGIDA

Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua kituo na kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UN women Tanzania Maria Karadenizli. 

Friday, January 20, 2017

WAZIRI UMMY AAGIZA WAKUNGA NA WAUGUZI WASIKAMATWE BILA YA KUFUATA TARATIBU ZILIZOPO.

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kuzindua  mradi wa Mkunga Okoa Maisha , wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada  Bi. Susan Steffan na wakawnza kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.

Thursday, December 15, 2016

MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam.

Friday, October 07, 2016

WAZIRI UMMY ATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA.

c1
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.

Thursday, October 06, 2016

WAKURUGENZI WATAKIWA KULIPA POSHO ZA SARE KWA WAUGUZI


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akiongea na wauguzi(hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 44 wa wauguzi Tanzania.

Wednesday, July 06, 2016

DK.KIGWANGALLA AFUNGA RASMI JUBILEE YA MIAKA 50 YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO JIJINI MWANZA.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.

Tuesday, May 17, 2016

DKT. KIGWANGALLA AWATAKA WANAFUNZI KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NCHINI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mku wa shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba wakati wa kuwasili katika eneo la Mahafali ya 19 ya kidato cha Sita ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Lushoto Tanga.

Monday, April 25, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUPIMA MALARIA KWA KUTUMIA MRDT:

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.

Friday, April 08, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD KANDA YA MBEYA.


Na Rabi Hume.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.

“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa.

“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.

Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e

Wednesday, April 06, 2016

MAMBO 9 MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU UKATILI KWA WATOTO:

Afisa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Asha Sarota akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. 
Mtangazaji Dominic Maro kutoka Redio Huruma akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. 

Thursday, March 17, 2016

WIZARA YA AFYA,YAZINNDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI HASA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango kazi wa Taifa wa dawa,vifaa tiba, na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kudhibiti wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji,mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde akifafanua jambo kwa waAndishi wa habari jinsi ya kuwezesha udhibiti wa wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imezindua mpango mkakati wa Taifa wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kuboresha huduma ya afya katika Halmashauri hizo.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye amesema kila dawa katika Halmashauri husika itakuwa na nembo pamoja na takwimu za watumiaji kwa lengo la kukwepa wizi wa dawa na kuwapa taarifa wawekezaji kwa kuweka viwanda vya dawa za binadamu.

Katibu Mkuu huyo,Bw.Ulisubisye ameongeza kuwa ukaguzi wa dawa utakuwa endelevu,usimamizi wa vifaa pamoja na kuona utoaji wa huduma za afya kwa mpango huo una ubora mkubwa.

Hata hivyo, Wizara ya Afya imeeleza kuwa mpango huo utadumu kwa miaka mitano hasa katika kutekeleza mpango wa dawa kupatikana katika kila Halmashauri pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watoaji huduma za afya.

Tuesday, March 01, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, DKT. HAMISI KIGWANGALLA AMEAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA ZA BINADAMU LA SHINE CARE PHARMACY LILOPO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.

Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.

Sunday, February 28, 2016

DR KIGWANGALA AWASHAURI WANANCHI KUWA NA TABIA YA KUPIMA AFYA YAO MARA KWA MARA.

 Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitoa hutuba fupi wakati wa tukio hilo la kambi maalum ya matibabu ya bure kwa wananchi wote iliyoandaliwa na Care Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mh. Mussa Hazan Zungu.

 Zoezi  likiendelea

Monday, February 01, 2016

WATUMISHI WA AFYA NCHINI WAMETAKIWA KUACHA KUHUJUMU DAWA ZINAZOPELEKWA KWA AJILI YA WANANCHI NA SI ZA BIASHARA KAMA WANAVYOFANYA

 
naibu waziri dkt.hamisi kigwangwala akiongea na watumishi hao
baadhi ya wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)kanda ya kaskazini wakimsikiliza naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani)

Monday, January 25, 2016

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 25 JANUARI 2016

Wizara yangu inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu 14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa pekee ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa Takwimu za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10 vimeripotiwa. Idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki iliyoishia tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621 na vifo 14 ambalo ni punguzo la asilimia (16%). Mkoa wa Morogoro bado umeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89, Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero 17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na Ilemela 13), Simiyu (Bariadi DC 29 na Bariadi municipal 23), Manyara (Simanjiro 48), Mara (Musoma Manispaa 11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita (Geita DC 21 na Geita TC 6)  na Mbeya (Kyela 26).
Mikoa mingine ambayo bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Dodoma (Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7), Kilimanjaro (6) na Kagera (2).

Friday, January 15, 2016

HUDUMA ZA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA HAPA NCHINI ZIMEKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEPO NA WATOA HUDUMA WASIOZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO MBALIMBALI.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, 
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
MAELEZO YA WAZIRI KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA
 
Ndugu Wananchi, Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. 

Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.