Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.
Kutokana na hali hiyo
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa
Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi
zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.
Mhe. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi
kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa
Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na
Mazingira ya rushwa.
Katika uchunguzi wa
awali uliofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mambo yafuatayo
yamegundulika:
(i) Ukiukwaji
wa Makusudi wa Sheria, Kanuni na Taratibu za
utoaji wa Leseni za Biashara.
(ii) Kutoa
Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa
kodi ‘Tax Clearance Certificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya Mapato.
(iii) Kukaa
na fomu za Wafanyabiashara 336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
(iv) Kukiuka
Mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa
Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi
yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.
Aidha, Mheshimiwa
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara wote nchini
watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha
urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais-TAMISEMI,
07
Januari, 2016.
No comments:
Post a Comment