Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana
Ramadhani Kailima akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo
pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhusu
masuala ya maadili na na ufanisi kazini kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana
Ramadhani Kailima akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC (hawapo
pichani) leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhusu
masuala ya maadili na na ufanisi kazini kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi.
Awataka kuzingatia maadili na Kanuni za Utawala bora na maadili
katika utendaji kazi,
· Awataka kuepukana na rushwa na kushinda
vishawishi vya rushwa.
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa
NEC kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi ikiwemo kuzingatia maadili
na kanuni za Utawala Bora na kuepukana na rushwa.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam
wakati alipofungua Mkutano wa Kumi na Mbili wa Baraza la Wafanyakazi na kuongea
na Wajumbe wa Tume hiyo pamoja na Wajumbe wengine wa TUGHE ngazi ya Taifa na
Matawi.
Jaji Lubuva amesema kuwa, Mabaraza ya Wafanyakazi
yameundwa Kisheria kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi ya Taasisi
ili kusimamia rasilimali pamoja na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi husika,
hivyo kufanyika kwa mkutano huo ni moja ya chachu ya kuboresha mazingira ya
kazi na kuongeza ufanisi na tija katika Taasisi hiyo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya rushwa, Jaji
Lubuva ameeleza kuwa, moja ya jukumu la NEC ni kuimarisha na kukuza demokrasia
na Utawala Bora, hivyo watumishi wa Tume hiyo hawanabudi kuzingatia maadili na
kanuni za utawala bora na maadili katika utendaji wa kazi zao pamoja na
kuepukana na vitendo vya rushwa na vishawishi vyake.
‘’Nimeambiwa kuwa, katika kikao hiki mtajadili
kuhusu mada mbalimbali kama vile Taratibu za Utendaji kazi Serikalini, masuala
ya uanzishaji SACCOS, Utekelezaji wa Bajeti na miradi ya Maendeleo, Ukimwi,
Bima ya Afya na masuala ya Madawa ya kulevya, niwaombe kujadili mada hizo kwa
kina na busara huku mkitambua kuwa matokeo ya majadiliano yenu ni kwa ajili ya
maslahi ya Taasisi yetu na Taifa kwa ujumla’’, alisema Lubuva.
Kwa upande mwingine, Jaji Lubuva amewataka
wajumbe wa Baraza hilo kujadili masuala ya afya kwa Wafanyakazi hususani suala
la ugonjwa waUkimwi katika sehemu ya kazi ambapo aliwaasa kila mfanyakazi
kujikinga dhidi ya janga hilo kwa kulinda afya yake na ya familia yake ili
Taifa liweze kunufaika na nguvu kazi iliyopo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhani Kailima ameitaka jamii kuondokana na
dhana potofu dhidi ya Tume hiyo kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu na chaguzi
ndogo zilizofanyika Tume hiyo imekuwa haina kazi ya kufanya mpaka uchaguzi
mwingine kwa kufafanua kuwa, Tume hiyo ina majukumu mengi hata baada ya
uchaguzi ikiwemo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Uandaaji na
Uratibu wa Kura za Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, Uratibu wa Marekebisho ya
Sheria ya Uchaguzi.
‘’Sio kweli kwamba Tume ya Uchaguzi mara bada ya
Uchaguzi Mkuu na chaguzi nyingine ndogo zilizofanyika kwamba ndo basi hatuna
cha kufanya, Tume ina majukumu mengi hata baada ya uchaguzi kama vile Uratibu
na Usimamizi wa Utungwaji wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Uundaji wa
Mpango Mkakati wa Tume, Uandaaji wa Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa wateja,
Usimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Tume na Usimamizi wa chaguzi ndogo pale
zinapojitokeza na Mrekebisho ya Muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi’’, alisema
Kailima.
Mkutano huo umefunguliwa leo ukiwahusisha
Watumishi wa Taasisi toka NEC, Wajumbe wa TUGHE ngazi ya Taifa na Matawi ambao
jumla yao ni 54.
No comments:
Post a Comment