Showing posts with label Arusha. Show all posts
Showing posts with label Arusha. Show all posts

Thursday, January 26, 2017

ASKARI WA SUMA JKT WATIWA MBARONI KWA KUUA WAFUGAJI WANNE NA KUJERUHI WATANO HUKO OLDONYOSAMBU MKOANI ARUSHA

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha, linawashikilia Askari wanne wa SUMA JKT kwa tuhuma za kuhusika kuwaua wafugaji wanne kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watano kwenye vurugu zilizotokea eneo la Oldobnyo Sambu wilayani Arumeru.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wafugaji wa kimaasai kuwavamia askari hao ambao walikuwa wamekamata ng’ombe ambao waliingizwa ndani ya msitu wa hifadhi ambao ni wa serikali, kwa ajili ya malisho, kutokana na ukosefu wa malisho.

Friday, June 10, 2016

WADAU MBALIMBALI MKOANI ARUSHA WAJITOKEZA KUCHANGIA ISAACK HABAKUKI KUSAIDIA KULIPA FAINI:

Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Sunday, February 28, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AWASILI MKOANI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na  Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Lekule Laizer.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga 

Thursday, January 21, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEWASILI MKOANI ARUSHA NA TAREHE 23 ATATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI WA KUNDI LA 57/15.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyhoYZRjbRLr-lZXpx3NaZY1vVTIuqNScZ-kp6HRo1f2gRn_4UOnROEYkkmhwte0wGQteJgNi_1MDnpu-JfxCSVTlxwY0VwQth9iaatHM66hjMATIUdheHb8Vhp8hIfbNv4UQgEfO_6Sqd/s1600/New+Picture+%25281%2529.png

Simu: 255-22-2114512, 2116898 
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              
Faksi: 255-22-2113425
                               
                              OFISI YA RAIS,
       IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Januari, 2016 amewasili Mkoani Arusha ambapo keshokutwa tarehe 23 Januari, 2016 atatunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli mkoani hapa.

Rais Magufuli amewasili Mjini Arusha akitokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es salaam na kupokelewa na mamia ya wananchi.

Akiwa uwanjani hapo Rais Magufuli amewashukuru wananchi kwa mapokezi makubwa aliyoyapata na amewaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi tu."Nawashukuru sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu" Alisema Rais Magufuli.

Akiwa njiani kutoka uwanja wa ndege wa KIA, Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa njiapanda ya KIA, Kikatiti, Usa River, Tengeru na Mount Meru Mjini Arusha ambapo huko kote pamoja na kusisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki ni kuchapa kazi, amewahakikishia kuwa hatawaangusha.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.

"Nataka niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa mafanikio" Alisisitiza Mheshimiwa Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema tayari serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu ya Msingi na Sekondari baada ya kufuta ada na akaonya kuwa watumishi wa umma hususani wakuu wa shule watakaothubutu kufanya ubadhilifu wa fedha hizo watashughulikiwa.

Amesema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka watanzania wote  kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.

21 Januari, 2016