Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa akionesha kwa waandishi wa Habari
picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe
Joseph Magufuli,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO
Bw. Raphael Hokororo.picha hiyo inauzwa sh. 15,000/- tu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akionesha
kwa msisitizo Picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa mkutano na Vyombo vya
habari leo Jijini Dar es salaam.
PICHA Rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuri imetoka leo Januari 8, 2015 katika
Ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa, amesema kuwa
Picha hiyo ya Rais Magufuri kwa kila moja itauzwa kwa sh15000 ya
kitanzania bila ya kuwekwa frem,huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere itauzwa kwa sh 5000.
Aidha Zamaradi amesema kuwa Nakala za picha
hizo zinapatikana Idara ya Habari Maelezo na Ofisi za Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA).
Picha hiyo ya Rais pamoja na ya Baba wa
Taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali,Taasisi za
Umma,Mashirika na Ofisi Binafsi.
Aidha Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
Maelezo Raphael Hokororo amesema picha ya Rais Magufuri imewahi kutoka mapema
sana kuliko picha za Waheshimiwa waliopita na kusema kuwa hairuhusiwi
kukopi wala kunakili picha hiyo.
Serikali inatoa onyo kwa wale wote
wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kusitisha matumizi ya picha
hiyo na wale wote wanaotengeneza picha ukubwa usio rasmi, hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.Kwani Idara ya Habari Maelezo ndiyo yenye Haki miliki
ya picha hiyo.
No comments:
Post a Comment