Mkuu wa Idara ya Mipango
Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara akisisitiza
jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kulia
ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na
Maendeleo ya Makazi George Pangawe na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu
ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji
na matumizi endelevu ya rasilimali kwa wananchi ili waweze kunufaika na
rasilimali zote zilizopo katika maeneo yao kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam
na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la
Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta wakati wa mkutano na vyombo vya Habari ikiwa
ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi
ya rasilimali ikiwemo ardhi.
Akifafanua Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo
itawasaidia wananchi kungamua na kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka kutumia
rasilimali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
’Elimu ya mazingira imejumuishwa katika
mitaala ya shule zetu hapa nchini ili kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya
rasilimali alisisitiza Mbuta
Akizungumzia faida za Elimu ya Mazingira
kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa itasaidia kujenga kizazi chenye uelewa
na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bw. George Pangawe alitoa wito kwa wananchi
kufuata taratibu zote za kisheria pale wanapotaka kuendeleza Kipande chochote
cha ardhi.
Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake
inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji wa ardhi na kuwataka
wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia Sheria na Kanuni
zinazosimamia Sekta ya ardhi.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mazingira pamoja na Halmashuri zote
nchini zimekuwa zikisisitiza kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya
rasilimali ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
No comments:
Post a Comment