Askofu
Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy
Mwalimu na Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
Katika
mkutano huo Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari
mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dkt.
Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na
swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje
ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia
mgonjwa.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la
Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza weledi wa
huduma za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam.
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa
pongezi hizo jana Ijumaa Januari 8, 2016 wakati akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo ambako alikuwa amelazwa kwa uchunguzi
wa afya yake na matibabu.
Alisema kwamba awali yeye alikuwa anaogopa
kutibiwa hapo kutokana na taarifa potofu zilizokuwa zinazotolewa kwenye vyombo
vya habari juu ya operesheni tata zilizowahi kufanyika katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, na kwamba sasa ameridhika kuwa ni vinginevyo kwani
Kitengo cha magonjwa ya moyo cha hospitali hiyo kimemdhihirishia kwamba kina
uwezo mkubwa wa matibabu ya moyo kama ilivyo hospitali zingine popote pale
duniani.
Askofu Mkuu huyo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi hiyo ya moyo
tangu Januari Mosi mwaka huu. Hali yake imeendelea kuimarika kila siku baada ya
kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu hapo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa
Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwa
ajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa nje ya nchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili,
Profesa Mohamed Janabi amesma kuwa Askofu Pengo ataruhusiwa mwisho wa juma hili
kwa kuwa afya yake imeimarika.
No comments:
Post a Comment