Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya Sanawali, Tekniko, Ngarenaro, Mbauda, Majengo Na Kisongo
Msafara wa Rais John pombe magufuli uliokuwa
ukielekea Monduli mapema leo umesimamishwa na wananchi katika eneo la Mbauda
lililopo ndani ya jiji la Arusha ili kushinikiza kutatua kero zao na changamoto
zao ikiwemo kuwepo na kiwanda cha mafuta ya kupikia cha Mount Meru Mill
kinachodaiwa kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Wananchi hao ambao walijikusanya kuanzia mida
ya saa mbili kamili asubui mbali na kumueleza Rais huyo kero zao, pia walitumia
nafasi hiyo kumpongeza kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu
yaliyopo humu nchini.
Akiongea mbele ya Rais mara baada ya kupewa
nafasi , mmoja wa wanachi wa eneo hilo la mbauda Thabiti Abubakari alimuomba
rais awasaidie kutatua tatizo la kiwanda hicho kutiririsha maji machafu ya
kiwandani kwani tatizo hilo ni baya na linawaharibia mazingira na kuhatarisha
afya zao .
‘’Musheshimiwa rais tunapenda utusaidie hapa
kwetu mbauda tuna kero kubwa inatusumbua, kuna hiki kiwanda cha mafuta ya
kupikia cha mount meru mill kimekuwa kinatiririsha maji machafu ya kiwandani
huku nje ambapo wananchi wanaishi , kiwanda hiki hakijajenga mitaro ya
kupitisha maji machafu hivyo maji yote machafu yakitoka huko kiwandani
yanaingia huku majumbani kwetu, hivyo muheshimiwa tunaomba utusaidie hili
tatizo kwani kiwanda hiki kipo ndani ya makazi ya watu,kinahatarisha afya sasa
inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao wanacheza uku mitaani
pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama kipindupindu maana maji haya ni
machafu sana”alisema Dhabiti
Akijibu swala hilo Rais magufuli alisema kuwa
amelisikia na aliwaagiza mamlaka ya usafi wa mazingira nemc kulifuatilia swala
hili mara moja .Aidha magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa jiji
la Arusha kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwahaidi ataendelea
kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa akifanya kampeni.
Alisema kuwa kipindi hiki akuja arusha kwa
ajili ya kuongea na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi arusha
kufanya mkutano mkubwa ambao pia atatumia mda huo kusikiliza kero za wananchi
wa jiji la hilo.
No comments:
Post a Comment