Showing posts with label Chadema. Show all posts
Showing posts with label Chadema. Show all posts

Monday, October 24, 2016

NDALICHAKO, MAHIGA WAWAVURUGA CHADEMA..... CCM WAJICHAGULIA MEYA BILA MPINZANI

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeususia uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hali iliyopelekea wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya uchaguzi peke yao na kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

CCM wamemchagua Benjamin Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho. George Manyama amepata Baraka za wajumbe hao wa chama tawala kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Chadema waliususia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM wamechakachua kwa kuwaleta Profesa Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu) na Balozi Agustine Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje) kupiga kura katika Manispaa hiyo ili hali waliapa na kusajiliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hivyo, sio wajumbe halali wa Kinondoni na hawakupaswa kupiga kura.

Wajumbe wa Chadema wanadai kuwa uchaguzi uliofanywa na CCM peke yao sio halali kwani pamoja na mambo mengine akidi ambayo ni 2/3 ya wajumbe waliopaswa kufanya uchaguzi huo kuwa halali haikutimia.

Chadema imepanga kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Monday, August 22, 2016

LOWASSA, MBOWE NA KATIBU MKUU CHADEMA WAANZA MIKAKATI YA UKUTA


Siku moja baada ya Chadema kutangaza safu ya Ukuta, viongozi wa chama hicho wameanza kutawanyika mikoani kuanza kutoa elimu ya mpango huo. 

Wakati mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alikuwa mkoani Mbeya na jana alishiriki ibada na kuanza vikao vya mkakati huo. 

Friday, January 08, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU VIKAO VYA TATHMINI NA UCHAMBUZI VYA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)



Katika utaratibu wake wa kujipanga na kuendelea kutekeleza mikakati ya malengo ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kufikia lengo kuu la kushinda uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa na utamaduni wa kuwa na vikao vya kujitathmini na kufanya uchambuzi kila baada ya uchaguzi mkuu na kuweka mpango kazi unaopaswa kutekelezwa na chama kwa miaka mitano inayofuata.