Tuesday, May 31, 2016

SHUKRANI

SIKILIZA KAZI MPYA 

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

WAZIRI WA AFYA MHE.UMMY MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI, TAREHE 31 MEI 2016


























Siku ya kupinga matumizi ya Tumbaku Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 31 Mei.Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku mwaka 2016 ni “jiandae kwa pakiti zisizo na matangazo wala vivutio”Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya kujiepusha au kujikinga na vivutio mbalimbali vya matangazo yanayo hamasisha matumizi ya sigara ambayo ina madhara mengi kiafya.

DPP AFUATILIA KITILYA NA WENZAKE KATIKA MAHAKAMA YA RUFANI

Mkurugenzi wa mashtaka Tanzania DPP Biswalo Mganga amemfuata Kitilya na wenzake katika mahakama ya Rufani ambapo ameongoza jopo la mawakili watano kutoka Jamuhuri na kuiomba mahakama ya rufani kutengua uamuzi  uliotolewa na mahakama kuu na iamuru mahakama kuu kusikiliza rufani hiyo.
Rufaa hiyo imesikilizwa na mahakama ya rufani Tanzania  mbele ya majaji wa tatu  Salim Masati,Agustin Mwarinja  na Musa kipenga,ambapo wamesikiliza hoja za pande zote mbili pasipo kutoa maamuzi .

JELA MIAKA 3 KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


Frank Mvungi

Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya mwanzo Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1 na 2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo ilifunguliwa mnamo tarehe 14/1/2016.

Akisoma hukumu  mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki, Hakimu Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

KATIBU MTENDAJI WA TUME YA VYUO VIKUU (TCU) PROFESA TUNUS MGAYA ALIYESIMAMISHWA KAZI NA WAZIRI WA ELIMU AFUNGUKA MAMBO MAZITO

ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

BUNGE LAWASIMAMISHA WABUNGE KWA KUFANYA VURUGU BUNGENI JANUARI 27 ,2016.



MAANDALIZI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA 2016/2017 YAANZA RASMI.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.

WAZIR MKUU MAJALIWA AWASILI ARUSHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha May 30, 2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa Kimataifa wa ‘Africa World Heritage’ kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YA CHINA YATOA MSAADA WA MADAWATI YA TSH MILIONI 20,

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida (kulia) akimkabidhi zawadi ya boga kubwa lenye zaidi ya kilo 7 balozi wa china nchini Tanzani Dr Lu Yong,ng baada ya kufanya ziara wilaya ya Iramba mkoa wa Singida na kutoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya Tsh milioni 20 , kushoto ni waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae ni mbunge wa Iramba pia akiwa ameshika boga la zawadi kwa balozi huyo( picha na matukiodaimaBlog) .

Monday, May 30, 2016

SERIKALI YATANGAZA KUSAFISHA SEKTA YA ELIMU HASA WALE WALOAJIRIWA KWA KUTUMIA VYETI BANDIA

Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa katika  sekta hiyo  wakitumia vyeti bandia .

Aidha, imewataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na mabadiliko makubwa ya kusafisha sekta ya elimu na utumishi wa umma yanayokuja nchini.

MH. WAZIRI :JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA WAFUGAJI:

Waziri wanchi,Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.January Makamba alitembelea Jamii ya wafugaji wa kimasai wanaoishi Mkoani Mrogoro,walayani Kilosa kata na kijiji cha Parakuyo. Waziri huyo aliwatembelea wafugaji hao kwa lengo la kuzungumza nao na kuwahamasisha wafugaji hao kuwasomesha watoto wao wa kike ili wapate elimu na kukomboa familia zao kielimu mara watakapoelimika.

ILIKUWA NI SIKU YA FURAHA MARA BAADA YA WAWILI KUUNGANISHWA NA KUWA MWILI MMOJA

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam leo May 28, 2016. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog -(Kajunason Studio).


Katibu Mkuu Mambo Ya Ndani Ya Nchi Afanya Ziara NIDA........, Atoa Habari Njema Kwa Watumishi 597 Walioachishwa Kazi

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA MSALATO – DODOMA ATEMBELEA MRADI WA KUPONDA KOKOTO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Stevin Mwihambi alipowasili Gerezani hapo kwa ziara ya kikazi.

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.

Friday, May 27, 2016

LOWASSA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPANI HAPA NCHINI

May 27 2016, aliyekuwa mgombea Urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Masahau Yoshida.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lowassa ameandika; "Nimekutana na rafiki yetu Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida, nikiwa pamoja na viongozi wote wa wilaya yetu ya Monduli.

NECTA SASA KUFUNGA MITIHANI KWA KUTUMIA MASHINE.




























Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejipanga kuanza kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani kwa kutumia mashine maalum ili kuondokana na hatari ya kuvuja kwa mitihani hiyo na gharama za ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/2017, jana Bungeni Mjini Dodoma.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JK IKULU JIJINI DAR:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MPYA WA COMORO.

Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi Comoro mara baada ya kuapishwa leo kwa kushinda uchaguzi mkuu wa April 10 na uchaguzi wa Marudio wa Mei 11 mwaka huu hafla ilifanyika  uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro

MTU MMOJA MKOANI MWANZA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.

Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA

 Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi  mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma kwenye viwanja vya Bunge.

WAZIRI PROFESA MAKAME ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE NA KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO

Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.

CHUMBA CHA DEREVA TAX KUWA GUMZO KWA WAKAAZI WA MBEZI.

Na Ripota wa Sufianimafoto ,Dar
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.

KIBITI KUFANYA KONGAMANO LA KUIPOKEA WILAYA MPYA KWA KUSHIRIKI SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO.

Na Daudi Manongi-MAELEZO

Viongozi wa umoja na wadau wa maendeleo wilaya mpya ya kibiti (UWAWAMAKI) mkoani Pwani umepanga kufanya kongamano la kuunga mkono tamko la Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuifanya Kibiti kuwa Miongoni mwa Wilaya mpya siku ya jumapili tarehe 29 saa nne asubuhi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari TEDEO Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Katibu wa umoja huo Bw.Selemani Ndumbogani  amesema kuwa wanakibiti wamefarijika sana na kauli ya Serikali ya Kuipatia Kibiti wilaya jambo ambalo lilikuwa kilio cha muda mrefu ikiwa ni takribani zaidi ya miaka arobaini tangu uhuru na kuongezea kuwa walikuwa mbali sana na huduma muhimu za Serikali.

MAHAKAMA YA TANZANIA INAKUSUDIA KUONGEZA IDADI YA MAJAJI KATIKA KANDA YAKE YA MWANZA:

chief-justice2
















Mahakama ya Tanzania inakusudia kuongeza idadi ya Majaji katika kanda yake ya Mwanza ili kuongeza msukumo wa kumaliza kesi za mauaji kutokana na kanda hiyo kuongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchi nzima.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ataongeza idadi ya majaji katika kanda hiyo ili kesi hizo za mauaji zimalizike kwa wakati.
Jaji Mkuu pia ameiagiza Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kuzipa msukumo maalum kesi za mauaji ili kuhakikisha zinamalizika mapema na kupunguza mlundikano wa kesi katika mahakama za Tanzania.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI WA HIFADHI ZA TAIFA NJE YA NCHI KWA MIAKA 3.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Baadhi ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.

VITA YA RUSHWA SI NGUVU YA SODA - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.
“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).

WAZIRI MKUU MSTAAFU NA MGOMBEA WA URAIS KUPITIA UKAWA EDWARD LOWASSA AFAFANUA JUU YA SHAMBA LA MAKUYUNI:


Siku chache  baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi unaomsafisha.

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MWANAHABARI MAKONGORO OGING' KUZIKWA MKOANI MARA KESHO KUTWA.


Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging' enzi za uwai wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging', Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging' wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam.

Thursday, May 26, 2016

MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI ATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU:

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake) alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.

MATUKIO YA BUNGEMJINI DODOMA 26/5/2016.

Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea leo mjini Dodoma.
BU2Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akifuatilia kwa makini michango ya wabunge wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu ndani ya Bunge mjini Dodoma.

RAIS DK.JOHN POMBE MAGUFULI AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA KWA WAKANDARASI:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano  wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tuesday, May 24, 2016

NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA KOMBE LA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI ( CDF CUP - 2016) JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

NAPE NNAUYE ASHINDWA KUHUTUBIA KWENYE TAMASHA LA MUZIKI JIJINI MWANZA KUTOKANA NA ZOMEAZOMEA YA WANANCHI WANAOTAKA BUNGE LIONYESHWE LIVE

Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU AG NA MSHAURI WAKE WA UCHUMI.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

BWANA GERSON MDEMU AMETEULIWA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU


PAPA FRANCIS AKUTANA NA WAISLAMU MISRI

Image captionPapa Francis akikutana na kiongozi mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu nchni Misri Al-Azhar
Kiongozi mmoja wa kidini nchini Misri amefanya mazungumzo na Papa Francis ,ikiwa ni ishara za hivi karibuni za kutaka kuimarisha uhusiano kati ya dini hizi mbili kubwa duniani.
''Mkutano huu ndio ujumbe'', Papa Francis alisema,huku akikutana na Sheik Ahmed el-Tayyib ,mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu cha Al-Azhar na Msikiti.