Tuesday, May 10, 2016

KESI YA GBAGBO YAANZA TENA KUSIKILIZWA ICC KWA WIKI MBILI:

Moja ya kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya ICC ambapo kesi katika Laurent Gbagbo inasikilizwa.
Moja ya kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya ICC ambapo kesi katika Laurent Gbagbo inasikilizwa.
REUTERS/Peter Dejong/Pool


Baada ya kusitishwa kwa wiki kadhaa, kesi ya Laurent Gbagbo inaanza upya Jumatatu hii katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire na mshirika wake wa karibu Charles Ble Goude wanafuatiliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Kikao hiki kipya kitadumu wiki mbili pekee, kwa sababu kesi nyingi zinatazamiwa kusikilizwa baada ya wiki hizi mbili. Wiki mbili ambazo upande wa mashtaka utaendelea kuwasilisha mashahidi wake.

Shahidi wa sita upande wa upande wa mashtaka anatarajiwa kusikilizwa Jumatatu hii. Kama kawaida katika Mahakama ya ICC, hakuna suala la kufichua utambulisho wake kabla ya kuanza kusikilizwa au kueleza kama atatoa ushuhuda wake hadharani au la.
Inajulikana hata hivyo kwamba atasikilizwa kuhusu nyaraka 85, ikiwa ni pamoja na video. Hadi sasa, waathirika wa mgogoro wamekutoa ushahidi wao, isipokuwa shahidi mashuhuri wa mwisho, "Sam l'Africain," kama anavyojiita, ambaye alionyeshwa na upande wa mashtaka kama shahidi muhimu, ambaye ataelezea mfumo wa ndani wa Laurent Gbagbo. Kwa kuunga mkono maelezo ya upande wa mashtaka kuhusu mpango wa mauaji uliyokua uliandaliwa kwa muda mrefu na rais wa zamani wa Côte d’Ivoire.
Jukumu la Ufaransa katika mgogoro wa Côte d’Ivoire
Lakini kama mfanybiashara wa Côte d’Ivoire mwenye asili ya Lebanon alitoa ushuhuda wake unaoweka wazi mpango wa mshirika wake wa karibu, pia kwa muda mrefu alimtetea Laurent Gbagbo. Katika hatua hiyo mwendesha alamua kusema kuwa mtu huyo ni "shahidi mwenye uhasama". "Sam l'Africain" alikuwa mmoja wa mashahidi wa nne ambao majina yao yalikua yalifichwa. hata hivyo utambulisho wao ulitangazwa na baadhi ya majaji mapema walipoanza kusikilizwa.
Suala jingine katika ajenda ya vikao hivi vya miezi hii ya kwanza ni kujua jukumu la Ufaransa katika mgogoro wa Côte d’Ivoire. Na si mshangao, wanasheria wa rais wa zamani wa Laurent Gbagbo wanaishutumu Ufaransa kujiingiza katika masuala yasiyoihusu. na hiyo ni moja ya ngao kuu ya utetezi wao.
Wakati hayo ya kijiri nchini Côte d’Ivoire kumefunguliwa Jumatatu hii Mahakama ya jadi itakayosikiliza kesi za uhalifu uliofanywa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na ile ya Simone Gbagbo. Mkee wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoireatahukumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Kesi hii mpya itaanza kusikilizwa mwishoni mwa mwezi Mei, kwa mujibu wa wanasheria wake na ina changamoto kwa vyombo vya sheria vya Côte d’Ivoire.

No comments:

Post a Comment