Showing posts with label Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Show all posts
Showing posts with label Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Show all posts

Tuesday, May 31, 2016

JELA MIAKA 3 KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


Frank Mvungi

Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya mwanzo Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1 na 2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo ilifunguliwa mnamo tarehe 14/1/2016.

Akisoma hukumu  mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki, Hakimu Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.