Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo katika kikao alichokiitisha kuhusu masuala ya madini kati yake na viongozi wa Serikali, viongozi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One na baadhi ya wachimbaji wadogo ,kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Februari 27, 2017.
Showing posts with label Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Show all posts
Showing posts with label Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Show all posts
Tuesday, February 28, 2017
Tuesday, February 07, 2017
DAWA YA MSONGAMANO WA MBAGALA YAPATIKANA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.
Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.
Wednesday, January 25, 2017
TUTAWASAKA NA KUWASHUGHULIKIA WALIOHUSIKA NA UPOTEVU WA MALI ZA KIWANDA CHA LUPEMBE-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inawasaka watu wote waliohusika na upotevu wa mali za kiwanda cha chai cha Lupembe na kuwachukulia hatua.
Hata hivyo amesema Serikali haitoipa nafasi migogoro yote ya uwekezaji inayopelekea wananchi kutopata ajira bali itatatuliwa bila ya kusimamisha uzalishali.
Thursday, January 05, 2017
WAZIRI MKUU AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA NA WATUMISHI KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa wasaidie kutoa utaalamu badala ya kupingana na madiwani ili wawezeshe kuleta maendeleo kwa wananchi.
Pia amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Wakuu wa Idara katika utekelezaji wa miradi iliyotengwa na Halmashauri.
Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mabada na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.
Tuesday, December 06, 2016
WAZIRI MKUU AMALIZA MGOGORO WA SHAMBA LA MANYARA RANCH KWA KUKABIDHI HATI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI,
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 17 kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei na Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) baada ya kukabidhi hati ya shamba la Manyara Ranch kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya.
Hati hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 4, 2016) na Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mto wa Mbu kwenye viwanja vya Barafu baada ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo vilivyopo kwenye Kata ya Elesilalei Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Thursday, September 29, 2016
Waziri Mkuu Atoa Mwezi Mmoja Kwa Watumishi Waliohamishiwa Kibiti Kuripoti Kituoni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Amesema mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo.
"Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo waishi Kibiti na si Ikwiriri," amesema.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya 74 waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti katika kituo cha kazi
Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano, Septemba 28, 2016 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo,utendaji wa serikali na kutoa msimamo wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wakuu wa idara ili kuepuka kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa kwa miradi mbalimbali ya jamii
Aidha aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha wawekezaji na wahakikishe kwamba uwekezaji utakaofanyika hausababishi migogoro ya ardhi kwa wananchi.
Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa maana Serikali imebeba mzigo wote wa gharama za ada na uendeshaji wa shule hizo.
Alisisitiza kuwa njia pekee na ya haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameagiza halmashauri zote nchini kutumia mfumo wa kieletroniki katika ukasanyaji wa mapoto ili kuziba mianya ya uvujaji mapato haswa ya maliasili
Saturday, September 24, 2016
WATUMISHI WA UMMA JIANDAENI KWENDA KUFANYA KAZI KOKOTE NCHINI-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kuwa tayari kwenda kufanya kazi kokote watakakopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika.
Amesema moja ya wajibu wa watumishi wa umma ni kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania sehemu yoyote walipo ili kuwaletea maendeleo na atakayeshindwa ni vema akatafuta shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mkunguni wilayani Mafia.
Wednesday, September 21, 2016
Thursday, August 25, 2016
MAJALIWA: WAKURUGENZI WAHAMASISHENI WALIMU KUJIENDELEZA KIELIMU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.
Tuesday, July 26, 2016
Friday, July 15, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA MADAKTARI WA KICHINA LUANGWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na madaktari wa Kichina ambao wako wilayani Ruangwa kwa ajili ya kupima na kuwatibu wananchi bure. Mazungumzo yao yalifanyika kwenye Ikulu ndogo ya wilaya ya Ruangwa Julai 15, 2016 . Kushoto kwake ni Naibu Balozi wa China nchini, Gou Haodong na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Wapili kushoto kwa Waziri Mkuu, ni Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya China na Tanzania(Tanzania Chinese Associanion), Joseph Kahama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu ).
Thursday, July 14, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO KATIKA KIJIJI CHA NANGUMBU WILAYANI LUANGWA
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na mkewe Mary wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nangumbu wilayani Luangwa baada ya kuwasili kijijini hapo wakiwa katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 14, 2016.
Wednesday, July 06, 2016
Friday, May 27, 2016
VITA YA RUSHWA SI NGUVU YA SODA - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.
“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).
Monday, May 16, 2016
MAJALIWA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo kuzungumza na watanzania waishio nchini humo Mei 14, 2016.. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa.
Tuesday, May 10, 2016
WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI LONDON
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kwenda London Uingereza Mai 10 , 2016, kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa kujadili masuala ya kupambana na rushwa duniani.(Picha n Ofisi ya Wziri Mkuu).
Wednesday, April 27, 2016
SERIKALI YAKIRI UPUNGUFU WA SUKARI, YAAGIZA NJE YA NCHI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.
Subscribe to:
Posts (Atom)







