ARDHI KUKUSANYA BILIONI 111.77 MWAKA UJAO WA FEDHA.
Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatarajia kukusanya shilini bilioni 111.77 kutokana na vyanzo mbalimbali za shughuli za sekta za ardhi katika mwaka ujao wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Alisema kuwa mapato hayo yanatarajiwa kupatikana kutokana upimamaji na ukutoaji hatimiliki za viwanja na mashamba 400,000 kwa wananchi.
Mhe. Lukuwi alisema kuwa maeneo mengine kuwa ni pamoja na wananchi kulipa kodi za ardhi na kutoza kodi ya ardhi kwa wenye leseni za vitalu vya kuchimba madini kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini.
DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 15.2 KUWAWEZESHA WANANACHI WA WILAYA KUMILIKI ARDHI.
Wakati huo huo jumla ya Dola Kimarekani milioni 15.2 zinatarajiwa kutumika kwenye mpango wa kuwezesha wananchi kumiliki ardhi ili kuwainua kiuchumi na kijamii.
Mpango huo unaotekelezwa katika wilaya ya Ulanga , Kilombero na Malinyi katika kipindi cha miaka mitatu ,umezindiliwa na Serikali kwa kushirikiana washirika wa maendeleo wa nchi za Uingereza, Sweden na Denmark.
Alisema kuwa zoezi hilo likifanikiwa nguvu zitaelekezwa katika wilaya nyingine hapa nchini ili kuongeza kasi ya kupima na kumilikisha ardhi kkwa wananchi.
Mhe. Lukuvi aliongeza kuwa kwa muda wa miaka mitatu , mpango huo utasaidia kutoa hatimiliki za kimila kiasi cha 300,000 na hati miliki za ardhi 25,000 katika maeneo ambayo mpango huo utakapokuwa unatekelezwa.
Alisema kuwa baada ya wananchi kupata hati hizo ,zinaweza kutumika kama dhamana ya kuwawezesha wakulima na wafugaji kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kujiendeleza na kupambana na umaskini.
Aidha , Waziri huyo alisema kuwa mpango huo utaongeza usalama na uhakika katika umiliki wa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
SERIKALI KUANDAA HATIMILIKI LAKI NNE NA ELFU 57 ZA KIMILA MWAKA UJAO WA FEDHA
Waziri ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali inakusudia kuandaa hatimiliki 400,000 na hatimiliki za kimila 57,000 katika mwaka ujao wa fedha.
Kufuatia hatua hiyo , aliziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha viwanja vyote vilivyopimwa na kuandaa hati ili wananchi waweze kuwa hati salama kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mhe. Lukuwi aliwaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa na wananchi kuhakikisha wanalinda miliki zinatolewa kisheria na maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya umma.
Aidha ,Waziri huyo aliliomba Bunge liidhinishe matumizi ya kawaida na maendeleo ya Wizara yake ya shilingi bilioni 61.8.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo matumizi ya kawaida ni bilioni 41.87 na bilioni 20.00 ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment