Monday, May 30, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA MSALATO – DODOMA ATEMBELEA MRADI WA KUPONDA KOKOTO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Stevin Mwihambi alipowasili Gerezani hapo kwa ziara ya kikazi.

mau2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akitoka katika lango Kuu la Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo Mei 29, 2016 Mkoani Dodoma(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja.

mau3
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kushoto) walipofanya ziara ya kikazi katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi.

mau4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisaini Kitabu cha Wageni kabla ya kupokea taarifa fupi ya hali ya Ulinzi na Usalama wa Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi  Mei 29, 2016.

mau5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo(katikati) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja kwa pamoja wakisikiliza kero mbalimbali za Wafungwa

mau6
Muonekano wa eneo la Gereza Msalato ambalo linajishughulisha na mradi wa upondaji wa kokoto kama inavyoonekana katika picha.

mau7
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano maalum na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa kuponda kokoto katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment