Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akizungumza na Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga,
wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam
leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za
kulenya nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Showing posts with label Mhandisi Hamad Masauni. Show all posts
Showing posts with label Mhandisi Hamad Masauni. Show all posts
Wednesday, February 22, 2017
Sunday, January 22, 2017
NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA GEREZA LA RUANDA JIJINI MBEYA
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida (kulia) wakati alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji thamani za ndani na sabuni katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Tuesday, September 27, 2016
MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Thursday, August 04, 2016
MHANDISI MASAUNI AZINDUA MKAKATI WA BARAZA WA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI NCHINI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
Thursday, July 14, 2016
WAZIRI MWAKYEMBE, MASAUNI WAFANYA ZIARA MKOANI GEITA, WAZUNGUMZA NA UONGOZI GGM, WATEMBELEA GEREZA CHATO
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya mkoani Geita (GGM) pamoja na Viongozi wa Serikali wa mkoa huo, kuhusiana na masuala mbalimbali ya utatuaji wa migogoro iliyopo kati ya GGM na wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo. Waziri Mwakyembe aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, katika ziara hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Thursday, June 23, 2016
NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AZUNGUMZIA MATUKIO YA KIHALIFU YALIYOTOKEA MKOA WA KUSINI PEMBA
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame.
Monday, June 13, 2016
SERIKALI YATANGAZA KIAMA KWA MAJAMBAZI NA WAUWAJI
Saturday, June 11, 2016
MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ATEMBELEA KITUO CHA POLISI KILICHOLALAMIKIWA BUNGENI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
Thursday, June 02, 2016
NAIBU WAZIRI MASAUNI ATUA MKOANI TANGA, AZUNGUMZA NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI, ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Monday, May 30, 2016
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA MSALATO – DODOMA ATEMBELEA MRADI WA KUPONDA KOKOTO
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Stevin Mwihambi alipowasili Gerezani hapo kwa ziara ya kikazi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
