Mkurugenzi
wa mashtaka Tanzania DPP Biswalo Mganga amemfuata Kitilya na wenzake katika
mahakama ya Rufani ambapo ameongoza jopo la mawakili watano kutoka Jamuhuri na
kuiomba mahakama ya rufani kutengua uamuzi
uliotolewa na mahakama kuu na iamuru mahakama kuu kusikiliza rufani
hiyo.
Rufaa hiyo
imesikilizwa na mahakama ya rufani Tanzania mbele ya majaji wa tatu Salim Masati,Agustin Mwarinja na Musa kipenga,ambapo wamesikiliza hoja za
pande zote mbili pasipo kutoa maamuzi .
Upande wa
Jamuhuri ukiongozwa na Mkurugenzi wa mashtaka DPP Biswalo Mganga, wamezitaja sababu za kukata rufani kuwa
ni, Jaji wa mahakama kuu, alikosea
kusema kuwa kufutwa kwa shtaka la 8 la utakatishaji fedha ,ni uamuzi mdogo,
pili Jaji, alikosea kusema kwamba, upande wa mashtaka ulikuwa na nafasi ya
kurekebisha mashtaka yao., lakini mahakama ya hakimu mkazi kisutu ilisha funga
milango ya kufanya marekebisho .
Na kwasababu
ya hoja hizo wameomba mahakama a rufaani kufuta uamuzi wa mahakama kuu, na
kuiamuru mahakama kuu kusikiliza upya rufaa hiyo.
Aidha kwa
upande wao mawakili wasomi upande wa utetezi,Majura magafu,dkt lingo Tenga na
Alex Mgongolwa wamesema kuwa, rufaa hiyo, iliyokuwa Imekatwa na upande wa
mashtaka, ilikua haija komaa,hivyo wangesubiri
hatua ya kusikilizwa ndipo wangekata rufani.
Wamesema
kitendo cha upande wa mashtaka kusema walikuwa na haki ya kukata rufaa,
wamesema kuwa, inaonyesha kuwa hoja hiyo ilikuwa na maombi ya kufanya mabadiliko.
Baada ya
hoja hizo DPP amewaambia majaji kuwa
mahakama kuu ilisema kuwa shauri hilo
lirudishwe Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, na kisutu ikasema kuwa imefungwa
mikono na mahakama kuu haijatoa maamuzi
hivyo inategemea Mahakam ya rufani itoe maamuzi.
Shitaka la
nane la utakatishwaji fedha linalo wakabili Hery Kitilya,Shose Sinare na Sioi Saimon liliondolewa
na mahakama ya hakimu Mkazi kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Amilius Mchauru, ambapo baada ya kuondelewa,
waendesha mashtaka walilikatia rufaa, katika mahakama kuu na mahakama kuu
kutolea maamuzi, kua rufaa hiyo haina miguu ya kusimamia hivyo kuwataka kurudi
mahakama ya kisutu.
Kitilya na
wenzake wamerudishwa rumande hadi mahakama ya rufani itakapotolea maamuzi
rufani hiyo.
Kutoka
katika mahakama ya Rufani jijiji Dar es Salaam Unique Maringo wapo radio FM.
No comments:
Post a Comment