Showing posts with label Edward Lowassa. Show all posts
Showing posts with label Edward Lowassa. Show all posts
Friday, March 03, 2017
Monday, August 22, 2016
LOWASSA, MBOWE NA KATIBU MKUU CHADEMA WAANZA MIKAKATI YA UKUTA
Siku moja baada ya Chadema kutangaza safu ya Ukuta, viongozi wa chama hicho wameanza kutawanyika mikoani kuanza kutoa elimu ya mpango huo.
Wakati mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alikuwa mkoani Mbeya na jana alishiriki ibada na kuanza vikao vya mkakati huo.
Wednesday, June 22, 2016
Lowassa Asaidia Watoto Yatima Dar es Salaam
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amewataka Watanzania kujali makundi ya watu wenye mahitaji maalumu hususan katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kauli hiyo aliitoa jana alipotembelea vituo vya watoto yatima jijini Dar es Salaam vinavyoendeshwa na Waislamu kwa lengo la kuwajenga watoto kiimani. Lengo la ziara yake ni kushiriki nao katika utekelezaji wa nguzo ya mfungo wa Ramadhan.
Tuesday, June 07, 2016
WAZIRI MKUU WA MSTAAFU AMBAYE PIA ALIKUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA AMEIBUKA NA KUWATAKIA MFUNGO MWEMA WAISLAM WOTE NCHINI.
Waziri Mkuu wa Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa Tiketi ya Chadema ameibuka na kuwatakia mfungo mwema waislam wote nchini.
Kupitia ukurasa wake wa facebook. Lowassa ameandika;
"Waumini wa kiislam Tanzania wanaungana na wenzao kote duniani katika kutimiza moja ya nguzo tano Za uislam kufunga Ramadhan.
Friday, May 27, 2016
LOWASSA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPANI HAPA NCHINI
May 27 2016, aliyekuwa mgombea Urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Masahau Yoshida.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lowassa ameandika; "Nimekutana na rafiki yetu Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida, nikiwa pamoja na viongozi wote wa wilaya yetu ya Monduli.
Subscribe to:
Posts (Atom)




