Waziri wanchi,Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.January Makamba alitembelea Jamii ya wafugaji wa kimasai wanaoishi Mkoani Mrogoro,walayani Kilosa kata na kijiji cha Parakuyo. Waziri huyo aliwatembelea wafugaji hao kwa lengo la kuzungumza nao na kuwahamasisha wafugaji hao kuwasomesha watoto wao wa kike ili wapate elimu na kukomboa familia zao kielimu mara watakapoelimika.
Aliwapa mfano wa viongozi wanawake mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa uwezo mkubwa hivyo akawaambia wafugaji hao kuwa iwapo watasomesha watoto wao wa kike watakuwa wameelimisha jamii ya wafugaji pia, kama anavyoonekana kwenye picha January Makamba akizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Parakuyo ambayo watoto wengi wanaosoma hapo wanatoka katika jamii ya wafugaji(PICHA NA IMANI SAMILA)
Hapa waziri January Makamba akizungumza na watoto wa kike kutoka familia za wafugaji katika kijiji cha Parakuyo.
Baadhi ya akina mama kutoka familia za wafugaji wakimsikiliza waziri January Makamba wakati alipokuwa akizungumza nao kijini Hapo.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
Waziri January Makamba akivishwa vazi la asili na wananchi wa kijiji cha Parakuyo kutoka jamii ya wafugaji.
Waziri January Makamba akiwashukuru mara baada ya kumvisha vazi hilo.
Waziri January Makamba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Parakuyo kutoka jamii ya wafugaji wakati alipowatembelea kijijini hapo
No comments:
Post a Comment