Tuesday, May 17, 2016

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AMEIOMBA TFF KUSIMAMIA LIGU KWA USTADI KULINGANA NA TARATIBU ZA MPIRA WA MIGUU

Na Beatrice Lyimo - MAELEZO

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Issaya Mwita ameiomba shirikisho la Michezo wa mpira wa miguu nchini (TFF) kuendelea kusimamia ligi kwa ustadi kulingana na ratibu na taratibu za mpira wa miguu kama zililivyoanishwa na Shirikisho la Soka Duniani( FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF).

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa Mstahiki Meya huyo inasema kuwa TFF inatakiwa kusimamia ligi hiyo ili kuainisha, kubainisha, kutajirisha na hatimae kutatua changamoto husika na kuwa na kiwango stahiki katika msimu unaofuata ukilinganisha na changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.

Aidha, ameipongeza klabu ya Yanga Africans Football Club kwa kunyakua ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya ishirini na sita(26) tangu kuanzisha kwa mashindano ya ligi kuu Tanzania yajulikanayo kama Vodacom Premier League.

Alifafanua kuwa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaiomba klabu hiyo kuthamini ubingwa wao kwa kuonyesha viwango vya kimataifa ili kufanya jiji kuwa chuo cha mafunzo ya michezo wa mpira miguu, bila kuridhika na kiwango walichonacho.

Mbali na hayo alitoa wito kwa wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kushirikiana ipasavyo ili kufanya ligi ya Tanzania iwe miongoni mwa ligi bora Barani Afrika na duniani kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment