Showing posts with label Profesa Joyce Ndalichako. Show all posts
Showing posts with label Profesa Joyce Ndalichako. Show all posts

Monday, October 24, 2016

NDALICHAKO, MAHIGA WAWAVURUGA CHADEMA..... CCM WAJICHAGULIA MEYA BILA MPINZANI

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeususia uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hali iliyopelekea wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya uchaguzi peke yao na kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

CCM wamemchagua Benjamin Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho. George Manyama amepata Baraka za wajumbe hao wa chama tawala kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Chadema waliususia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM wamechakachua kwa kuwaleta Profesa Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu) na Balozi Agustine Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje) kupiga kura katika Manispaa hiyo ili hali waliapa na kusajiliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hivyo, sio wajumbe halali wa Kinondoni na hawakupaswa kupiga kura.

Wajumbe wa Chadema wanadai kuwa uchaguzi uliofanywa na CCM peke yao sio halali kwani pamoja na mambo mengine akidi ambayo ni 2/3 ya wajumbe waliopaswa kufanya uchaguzi huo kuwa halali haikutimia.

Chadema imepanga kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Tuesday, May 31, 2016

KATIBU MTENDAJI WA TUME YA VYUO VIKUU (TCU) PROFESA TUNUS MGAYA ALIYESIMAMISHWA KAZI NA WAZIRI WA ELIMU AFUNGUKA MAMBO MAZITO

ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

Friday, May 20, 2016

MAJALIWA AKUTANA UJUMBE WA CHUO KIKUU CHA AGHA KHAN

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chuo Kikuu cha Agha Khan, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Mai 19, 2016. Kutoka kushoto ni  Al – Karim Haji, Firoz Rasul, Joel Lugallo na Amin Kurji. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)