Thursday, May 19, 2016

WAKUU WA MIKOA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE.

Wakuu wa Mikoa wakiwemo wakuu wa wilaya waliowakilisha mikoa yao wakiwa katika ofisi za Shirika za Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kimafunzo katika Hifadhi ya TAifa ya Tarangire.

Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya wakiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa maelezo mafupi kwa Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya kabla ya kuanza safari ya kutembelea Hifadhi ya Tarangire.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara aliyekuwa mwenyeji wa wakuu wa mikoa hao,Joel Bendera akitoa neno la ukaribisho kwa wageni hao baada ya kufika katika Hifadhi ya Tarangire.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akichukua taswira wakati viongozi hao wakitembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyoko mkoani Manyara.
Kivutio kimojawapo ni Ndege katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Kundi la Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Wakuu wa mikoa wakitizama wanyama.
Mnyama Ngiri katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Tumbili na mtoto wake mgongoni katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya wakitizama eneo moja wapo la chanzo cha Mto Tarangire.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Mecky Sadick walipokuwa wakitizama sehemu ya chanzo cha Mto Tarangire.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Susuma Kusekwa akitoa maelezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya waliotembelea hifadhi ya taifa ya Tarangire.
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Wasaidizi wa wakuu wa Mikoa wakiwa katika picha ya pamoja katika Hifadhi ya taifa ya Tarangire.
Mnyama aina ya Kuro katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ambaye pia ni Raisi wa Shirikisho a Riadha Tanzania akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero,Betty Mkwasa ambaye pia ni mke wa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ,Charles Mkwasa wakiwa ni miongoni mwa viongozi waliotembelea Hifadhi za Taifa Tarangire.
Wakuu wa Mikoa wakiwa katika moja ya hoteli zilizopo katika Hifadhi ya hiyo,Tarangire Safari Lodge wakitizama wanyama waliokuwa wakivuka mto.
Kundi la Tembo likivuka mto .
Mandhari ya kuvutia ikionekana baada ya kufika katika Hotel ya Tarangire Safari Lodge.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky saidick pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Mhuga wakitizama bidhaa katika moja ya maduka yaliyopo katika Hoteli ya Tarangire Safari Lodge.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali ,Raphael Mhuga akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya wenzake kwa uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) baada ya kuhitimisha ziara ya kimafunzo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment