Frank
Mvungi
Mahakama
ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya mwanzo
Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba na kupokea
Rushwa kinyume na kifungu cha
15 (1 na 2) cha
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Kwa
Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo ilifunguliwa mnamo
tarehe 14/1/2016.
Akisoma
hukumu mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki, Hakimu Hakimu
Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa ushahidi
uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka umethibitisha
pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Ilisisitiza Sehemu ya
Taarifa hiyo kuwa kwa mujibu wa ushahidi Mtuhumiwa aliomba kiasi cha Tshs.
300,000/= na kupokea kiasi cha Tshs. 100,000/- kutoka kwa Bw. Reuben Francis
Ndimila ili asimkamate mtuhumiwa aliyeruka dhamana. Taarifa hiyo imeongeza kuwa
Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa katika makosa hayo mawili ya kuomba na
kupokea hongo.
Aidha
Mh. Kato akitoa adhabu kwa Mshitakiwa alisema, Mshitakiwa anatakiwa kutumikia
kifungo cha miaka Mitatu (3) jela au kulipa faini ya Tshs. 600,000/= kwa kila kosa.
Mshitakiwa amepelekwa jela kuanza kutumikia adhabu hizo kama
zilivyotolewa.
Kesi
hiyo ilisajiliwa mahakamani hapo kama kesi ya Jinai Na. 18/2016 na kusikilizwa
na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoa wa GEITA Bw. Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya
ya Chato kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya Rushwa na ubadhilifu katika
miradi mbalimbali ya maendeleo na maeneo mengineyo ili watuhumiwa waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment