Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.