Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson (katikati ya waliokaa) katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar wakiongozwa Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid (wa pili toka kulia).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Akcson amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ulioongozwa na Spika Mhe Zuberi Ali Maulid na kuahidi kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina na Vyombo hivyo viwili vya kutunga sheria.
Akizungumza na ugeni huo uliomtembelea kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi Naibu Spika amesema ili mahusiano ya Vyombo hivi viwili yaboreke zaidi kuna haja ya kuwa na mafunzo ya pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ambazo nyingi zinafanana.
Naibu Spika aliongeza pia kuwa Bunge la Jamhuri ya Muuumgano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni Vyombo vinavyofanya kazi zinazofanana hivyo kujifunza na kubadilishana uzoefu ni jambo la muhimu katika katika kuboresha utendaji kazi.
“Mahusiano tuliyonayo yanawekewa nguvu tunapokuwa na mafunzo yale ya pamoja kwa sababu fursa inapatikana ya kubadilishana uzoefu lakini pia kujifunza mambo kwa pamoja kuliko kukiwa na uendeshaji ambao ni tofauti sana wakati Vyombo hivi vinafanya kazi inayofanana,” alisema Naibu Spika wakati akizungumza na Ugeni huo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Dkt Tulia pia ametumia fursa hiyo kumpongeza Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuchaguliwa kushika nyadhifa hizo na kusema kuwa Bunge lipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote utakapohitajika.
Kwa upande wake Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid amesema Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kitu kimoja hivyo wameona ni muhimu kuja kusalimiana, kufahamiana na kuimarisha mahusiano yaliyopo ili kurahisisha utendaji kazi wa Vyombo hivyo.
Adiha alisema kuwa Baraza la Wawakilishi litaendelea kujifunza na kuomba ushauri toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ili hilo lifanikiwe kuna haja ya kuboresha zaidi mahusiano ya mihimili hiyo miwili ya kutunga sheria.
Pia Mhe. Maulid amempongeza Naibu Spika Dkt Tulia kwa umahiri wake wa kupambana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uendeshaji vikao vya Bunge na kusema kuwa kuna mambo mengi wamejifunza kutoka kwake. Pamoja na Watendaji wengine wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Spika wa Baraza hilo aliamabatana pia na Naibu Spika wa Baraza Mhe Mge
No comments:
Post a Comment