Waandishi wa habari wakimsikiliza bwana Bwana Mbuso Dlamini katika maadhimisho ya miaka kumi ya taasisi hiyo
mkurugenzi Dr Ellen Otaru Okoedion akitoa ufafanuzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya taasisi hiyo ya Faidika kwa waandishi wa habari hawapo pichani.
Katikati ni mkurugenzi mkurugenzi Dr Ellen Otaru Okoedion na afisa mtendaji mkuu Bwana Mbuso Dlamini akielezea mwonekano mpya wa Rangi na logo ya taasisi hiyo ya faidika.
Na Anaseli Stanley
Kampuni ya
letshego tanzania limited ikijulikana kama Faidika imesheherekea miaka 10 ya
utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini na kuzindua upya safari ya mabadiliko
na msukumo wa ujumuishaji kwenye sekta ya kifedha kwa lengo la kuboresha maisha
ya wananchi wa tanzania
Akizungumza
kwenye hafla hiyo afisa mtendaji mkuu wa faidika Bw. Mbuso Dlamini amesema
wataendelea kutoa ufumbuzi wa kifedha utakaoboresha maisha na kuhakikisha
ufumbuzi huo unaleta maana kwa watanzania .
Aidha
Bw.Dlamini amesema watashirikiana na serikali kuwajengea ujuzi wananchi na
kuhamasisha mahusiano ya kimkakati kwa lengo la kumwinua mtanzania mwenye
kipato cha chini pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiria mali kwa wajasiriamali
wadogo wadogo.
‘Ili
kufanikisha lengo la ujumuishaji wa kifedha faidika imeanzisha ufumbuzi
wenye lengo la kuboresha maisha
kupitia upatikanaji wa mikopo ya kilimo
,elimu, afya na nyumba kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati na
wajasiriamali wadogo’, alisema Dlamini.
‘ Uzinduzi
huu unakazia ahadi mpya ya Faidika isemayo Tuboreshe maisha’.aliongeza Dlamini.
Faidika imefanikiwa kuwafikia zaidi ya watanzania
45,000 nchi nzima ambapo wmenufaika katika maswala ya kifedha kutoka na huduma
hizo kutolewa kwa urahisi, stahiki na kwa unafuu zaidi.
Letshego ni
taasisi inayotoa huduma za kifedha ambayo imejitolea kuendeleza ujuzi na vipaji
na ina zaidi ya vituo vya uwakilishi 268 kupitia mitandao yake inayohudumia
zaidi ya wakopaji laki tatu na wawekaji
laki moja .
No comments:
Post a Comment