Showing posts with label waziri wa nchi. Show all posts
Showing posts with label waziri wa nchi. Show all posts
Friday, December 02, 2016
Thursday, July 14, 2016
JK - UTAFITI WA KINA WAHITAJIKA KATIKA KUKUMBANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI AFRIKA

Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa tatu wa Sera za Mabadiliko ya Tabia Nchi jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Climate Strategies. Mkutano huo ilijumuisha watafiti na watunga sera 80 kutoka nchi zaidi ya 10 nje na ndani ya Afrika chini ya kauli mbiu "Kutekeleza Makubaliano ya Paris - Suluhu Mpya za Utafiti kwa ajili ya Nchi zinazoendelea." Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Chuks Okereke, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja.

Thursday, May 19, 2016
Friday, March 18, 2016
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA TASAF NA TUME YA UTUMISHI WA UMMA:
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Ladislaus Mwamanga akiwasilisha mada ofisini kwake wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa mchango wake wakati wa kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa .
Thursday, January 07, 2016
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE (MB) AMEMUAGIZA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILALA KUMSIMAMISHA KAZI KAIMU AFISA BIASHARA WA MANISPAA YA ILALA BW. DENNIS. N. MREMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.
Kutokana na hali hiyo
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa
Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi
zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.
Mhe. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi
kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa
Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na
Mazingira ya rushwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)