Monday, July 04, 2016

SHRIKA LA TAIFA LA BIMA (NIC ) KUANZISHA BIMA YA KILIMO


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango- Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano , Mwanaidi Shemweta. NIC ilishiriki maonyesho ya 40 katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere maarufu kama sabasaba kama ilivyo desturi ili kutoa elimu kwa umma kuhusiana na maswala ya Bima. Pamoja na kutoa Elimu NIC imepata fursa ya kuelezea bidhaa mpya zilizokwishaanzishwa pamoja na zile mpya zinazotarajia kuanzishwa hususani Bima za KILIMO. Wananchi wanakaribishwa kuja kupata elimu hizo.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango-Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akitia saini kitabu cha wageni ndani ya banda la NIC baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalamu wa maswala ya Bima NIC.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Bw. Elisante Maleko Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja baada ya kutembelea na kupata maelezo yahusuyo maswala ya Bima ndani ya banda la NIC. Wakuu hawa wameona umuhimu wa Bima zitolewazo na NIC na wamesisitiza swala la Elimu liwe endelevu ili jamii ya kitanzania ipate uelewa na hatimaye kukatia bima hizo kwa manufaa ya familia zao.

No comments:

Post a Comment