Showing posts with label katibu wake mkuu. Show all posts
Showing posts with label katibu wake mkuu. Show all posts

Friday, July 22, 2016

MAALIM SEIF KUTINGA MAHAKAMA YA ICC KUWASHITAKI VIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA:

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa. 

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.