Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya .
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
SERIKALI imezuia taasisi za fedha (Benki) pamoja na kampuni za simu za mikononi kutoza ongezeko la thamani (VAT )kwa walaji (wananchi).
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidatta amesema kuwa fedha ambayo walikuwa wanakata haina ongezeko la thamani hivyo taasisi za fedha (Benki) kampuni za simu zimetakiwa zisiongeze miamala kwa wateja kwa kizingizio cha ongezeko la thamani.
Amesema kuwa fedha iliyokuwa ikikatwa imekuwa haikatwi hivyo kwa sheria hiyo inataka miamala hiyo iliyokuwa ikikatwa ikatwe asilimia 18 ya thamani ya ongezeko.
Aidha amesema TRA haijaweka muongozo wa juu ongezeko hilo kwa taasisi za fedha na kampuni za simu, hivyo kwa watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.
Kidata amesema kuwa wananchi wametakiwa wasiguswe kabisa katika ongezeko hilo kutokana na kutohusika na kufanya hivyo ni makosa.
No comments:
Post a Comment