Thursday, July 14, 2016

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI WAKATI WA UZINDUZI WA MPANGO WA UGAWAJI MADA...


1-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao ambapo pamoja na kuishukuru ofisi ya Bunge kwa kazi hiyo pia ameahidi serikali yake kuendelea kukabiliana na changamoto zilizokatika sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia. Katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.

2-Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao ambapo alisema ofisi ya bunge inatarajia kugawa jumla ya madawati 61,385 katika majimbo 155 kati ya majimbo 264 ambapo ni sawa na asilimia 59 wa madawati 120,000 yanayotarajiwa kutengenezwa na ofisi hiyo Leo katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mstahiki Meya Isaya Mwita akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini.
4- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya watoto wa shule ya msingi bunge wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
5- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua madawati katika mfano wa Darasa wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam. Anayemfuata ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
6- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Idd Azzan Madawati yaliyotolewa na Ofisi ya bunge kwa ajili kwa niaba ya wabunge waliopata mgao huo katika awamu ya kwanza.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
7-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
8- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka shule ya msingi bunge iliyopo Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
9- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Diwani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mstahiki Meya Isaya Mwita na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments:

Post a Comment