Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva - Switzarland, Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kwa lengo kuwajengea uwezo watalaam kuhusu ujazaji wa taarifa kuhusu sababu ya kifo cha mgonjwa pindi wanapojaza cheti cha kifo (Death Certificate).Washiriki wa Mafunzo hayo ya Siku mbili watakua na jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi wanazotoka kuhusu mfumo huo.
Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.
Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania na Malawi wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya mwisho ya kifo cha mgonjwa jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.
No comments:
Post a Comment