Kamanda Simon Sirro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Kamanda Simon Sirro akionesha silaha
Picha na habari na Anaseli Stanley,
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama wameweka mikakati ya mpango kazi wa kudhibiti matukio ya uhalifu au fujo katika kusheherekea sikuu ya Id El fitri.
Akizungumza na waandishiwa habari jijini Dar es salaam kamishna wa kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Siro amesema wataweka vituo vya polisi sehemu zote ili kuhakikisha kuwa watu wanasheherekea siku hiyo kwa usalama.
Kwaupande mwingine kamanda Siro amesema jeshi la polisi imekusanya zaidi ya shilingi milioni mia tatu za tozo ya makosa ya usalama wa barabarani kuanzi juni 30 hadi julai 4 mwaka huu.
Kamanda Siro ameongeza kuwa wanefanikiwa kukamata bastola iliyotengenezwa kienyeji katika eneo la mburahati barafu ambapo imebainika kuwa silaha hiyo ilikuwa ikitumika katika matukio ya unyanganyi.
No comments:
Post a Comment