Showing posts with label uwanja wa ndege wa Dodoma. Show all posts
Showing posts with label uwanja wa ndege wa Dodoma. Show all posts

Tuesday, July 12, 2016

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA KASI YA UPANUZI WA UWANJA WA UWANJA WA NDEGE, DODOMA



















Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa na maendeleo ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 35 ikiwa ni kazi iliyotekelezwa ndani ya siku 18 toka alipotoa agizo hilo mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu. 

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja huo na kumhimiza mkandarasi wa Kampuni ya Chico kuendeleza kasi ya ujenzi huo ili kukamilisha kwa wakati uliopangwa na kutoa msisitizo kwa makandarasi wengine wanaotekeleza miradi mbalimbali nchini kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukamilisha miradi hiyo kwa muda mfupi kulingana na makubaliano ya mikataba.